test
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KITAIFA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KITAIFA. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 4 Januari 2019

Jumanne, 31 Julai 2018

Habarika Masaa 24......Pakua Application Yetu Tukuhabarishe Usiku na Mchana


Jumamosi, 16 Juni 2018

Breaking News: Orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha TANO, Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Elimu ya Kati kwa mwaka 2018


Wanafunzi 70,904 waliohitimu kidato cha nne mwaka jana wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vya elimu ya kati kwa mwaka 2018, huku wengine 21,808 waliokuwa na sifa za kuchaguliwa wakiachwa.
==>>Orodha Yote ya Majina iko hapo chini
NB:  Server iko bize kidogo, endelea kurefresh kama itakuwa inagoma kufunguka

Read More

Jumatatu, 11 Juni 2018

Rais Magufuli Amteua Bw.fidelis Mutakyamirwa Kuwa Mwenyekiti Baraza La Taifa La Ushauri Wa Ardhi


Read More

Binti wa kazi aliyemuua Boss wake na Mwanae Amekamatwa


Mfanyakazi wa ndani aliyemuua mwajiri wake pamoja na mtoto wake mwenye miezi mitatu huko Muhoroni, Kisumu nchini Kenya na kutokomea kusikojulikana amekamatwa Uganda na jeshi la polisi la nchi hiyo.

Jacky Auma alikamatwa katika eneo la Namayisi nchini Uganda baada ya jeshi la Polisi nchini Kenya kuwapa taarifa juu ya mtuthumiwa huyo kukimbilia katika mipaka ya nchi hio.

Jacky anatuhumiwa kutenda tukio hilo wiki iliyopita kwa kumpiga mtoto wa mwajiri wake mpaka kufa kisha akamchoma mwajiri wake na kisu mara kadhaa kabla ya kumchoma na kitu kinachodhaniwa kuwa ni pasi ya umeme au tindikali na kumfanya apoteze uhai wake.

Aidha Afisa Polisi wa kituo cha Busia amethibitisha kukamatwa kwa Jacky na amesema kuwa wako wanaandaa utaratibu ili mtuhumiwa huyo arudishwe nchini Kenya akafunguliwe mashitaka.

Read More

Jumapili, 10 Juni 2018

Jambazi maarufu kwa jina la Rambo auawa na wananchi


Mtuhumiwa wa ujambazi anayedaiwa kuteka magari na kunyang'anya mali za watu wanaotumia barabara ya Kisili - Buhigwe mkoani Kigoma maarufu kwa jina la ‘Rambo’ ameuawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mtuhumiwa huyo ameuawa akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Wilaya Kasulu kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa wananchi wenye hasira.
Ottieno amesema Rambo alikamatwa katika Kijiji cha Bukuba, Kata ya Janda wilayani Buhigwe akiwa katika harakati ya kuteka magari na watu wanaopita barabarani.

"Kwa kuwa tumehamasisha jamii kumkabili huyo Rambo kwa vile anatumia bunduki za bandia, watu walipomuona waliamua kumkabili na wakamdhibiti kikamilifu kabla ya kutupigia simu (Polisi)," amesema.

Rambo alikuwa raia wa Burundi anayetoka jimbo la Makamba, lakini aliingia Kigoma kwa njia za panya kinyume cha sheria na alikuwa akitumia bunduki bandia zilizochongwa kwa ustadi akitumia mbao na kuviringisha vitambaa ili kuwahadaa watu anaowateka alikuwa tishio kutokana na kuwakwepa polisi mara mbili.

Credit: Mwananchi
Read More

Mama Amuua Mtoto Wake Kwa Kumkaba Shingoni na Kisha Kumtupa Mtoni


Polisi Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata Mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumkaba shingoni mtoto wake wa miaka 5 na kisha kumtupa katika mto Rutui.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa Mwanamke huyo mwenye miaka 23 ambaye anaishi peke yake, baada ya kutenda tukio hilo alimtupa mwanae kwenye mto na kukaa kimya akiamini kuwa maiti ya mtoto wake itachukuliwa na maji na kupelekewa sehemu isiyojulikana.

Duru za kuaminika zinasema kuwa ndugu wa mtuhumiwa huyo walianza kumuulizia mtoto  na mtuhumiwa akawa anawajibu  kuwa na  yeye anashangaa kutoweka kwa mwanae.

Aidha mwili wa mtoto huyo ulionekana ukielea katika mto Rutui asubuhi ya June 9 na ndipo wakazi wa eneo hilo ikiwemo mtuhumiwa waliwaita Polisi na kuutoa mwili wa mtoto huyo kisha wakamkamata mtuhumiwa.

Kwa mujibu wa Polisi wa kituo cha Kirinyaga Yaya Chome amesema kuwa mwanamke huyo amefunguliwa mashitaka ya kusudio la kutaka kuua katika mahakama ya Kerugoya.

Chanzo cha mama huyo kutenda tukio hilo la kinyama bado hakijawekwa wazi.
Read More

Ijumaa, 8 Juni 2018

Sakata la KKKT Lamfukuzisha Kazi Msajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu Nchemba amesimamisha kazi Msajili wa Taasisi za Dini Maryline Komba huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea na shughuli zao za kutoa huduma za kiroho.
 
Waziri Mwigulu ameyasema hayo wizarani hapo wakati alipotangaza kumsimamisha kazi na  kupisha uchunguzi wa kina na iwapo atabainika kutohusika na matamko hayo au nyaraka ambazo zinasambaa mtandaoni basi atarudi kwenye majukumu yake.
 
Wizara yake inaendelea kuchunguza aliyeandika na kusambaza nyaraka katika mitandao ya kijamii ambayo imeibua sintofahamu kwa viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla ili sheria ichukue mkondo wake.
 
“Serikali na viongozi wa dini wamekuwa na ushirikiano mkubwa na hakuna mahali ambapo wanaonekana kutoaminiana.Hivyo aliyesambaza nyaraka hizo tunachunguza na kisha tutachukua hatua zinazostahili,”amesema Dk.Mwigulu.
 
Amesema viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla wafahamu kuwa nyaraka na matamko ambayo yamesambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina baraka za Wizara yake wala Serikali na hivyo ni vema zikapuuzwa tu.
 
Amewaomba  viongozi wa dini kupuuza nyaraka  zinasambazwa kwenye mitandao na kusema “Endeleeni na shughuli zenu kama kawaida kwani nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria hivyo hakuna sababu ya kuhofu.
 
Amesisitiza kuwa Serikali inaheshimu viongozi wa dini zote huku akionya wanaotaka kutumia dini kama kigezo cha kufanya siasa au kuigawa nchini.
 
“Wale ambao wanataka kutugawa kwa misingi ya kidini ni vema wakaacha kwani haitakuwa na tija kwao wala kwa Taifa letu .Hivyo tusiwe sehemu ya kushabikia mambo yanayohusu dini,”amesema.
Read More

Mrema Ammwagia Sifa Diamond


Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema amesema msanii wa Bongo Flava anayemfuatilia kwa sana ni Diamond Platnumz.

Ameeleza sababu ya kumfuatilia muimbaji huyo ni kutokana na kujituma kwake na muziki wake unavutia.

“Namfuatilia sana Diamond, ni kijana mdogo, muimbaji mahiri, yaani Diamond asaidiwe naona hatima yake katika maisha yake na nchi yetu atatufikisha mahali pazuri. Kwa muziki wake unakosha roho, hata sisi wazee, mimi naridhika sana,” Mrema ameiambia Times FM.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa serikali kuwa karibu zaidi na wasanii, hata hivyo amesema anaziona jitihada za Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe za kukutana na wasanii kila mara hasa pale wanapopata matatizo na kuwasaidia.
Read More

Dr Shika Kaja Kivingine...Leo Kamtambulisha Msanii Wake Anayemsimamia


Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, amefunguka na kutangaza nia ya kujihusisha na masuala ya muziki nchini Tanzania hasa upande wa kuwasimamia wasanii wachanga na wakubwa.

Dkt. Shika ametoa kauli hiyo leo Juni 08, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema siku si nyingi atatangaza jina rasmi ya label yake ambayo itakuwa inajuhusisha na kusimamia kazi za wasanii wa BongoFleva huku akidai lengo lake kubwa ni kutaka kutimiza ndoto za kila mmoja kupitia sanaa.

"Sasa tutaelewana tu na kabla hatujaanza na masuala ya viwanda 30 nilivyo vitaja na 'different services', kwa sasa ninaanza na 'music industry' na tunaanzia kwa msanii mmoja ambaye anaitwa Godson anayetokea Songea na hili nina uhakika watanzania watafurahi na kufuta 'stress' mbalimbali zilizokuwa zinawasumbua", amesema Dkt. Shika.

Pamoja na hayo, Dkt. Shika ameendelea kwa kusema "nipo tayari kuwasimamia wasanii wengine watakaopenda lakini ninaanza na huyu mmoja na nina uhakika atawafunika wasanii wengi, kwa hiyo jaribuni kumfuatilia".

Kwa upande mwingine, Dkt. Louis Shika amesema ukimya wake wa kipindi kirefu umetokana na yeye kuhangaikia kuingiza fedha nchini kutokea nje ili aweze kutimiza azma yake aliyokuwa ameitangaza hapo awali.
Read More

Waziri Mwijage Aipongeza Kampuni Ya Total Kwa Kuzindua Mafuta Ya Magari Rafiki Kwa Mazingira


Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya mafuta ya TOTAL kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kuwa watanzania wanapata mafuta bora ya vyombo vya moto.

Mwijage alizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mafuta ya vyombo vya moto aina ya TOTAL Excellium kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL. Mafuta hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya ubora wa juu ya kimataifa ya TOTAL EXCELLIUM, kwa bidhaa zinazotumia mafuta ya Petroli na Diesel katika soko la Tanzania.

“Uzinduzi wa mafuta haya umekuja wakati muafaka kwani sasa tuko kwenye wiki ya mazingira na mafuta haya yanapunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na vyombo vya moto, nawapongeza kampuni ya TOTAL kwa kuwaletea watanzania bidhaa bora, na mimi na utaalamu wangu wa mafuta nafahamu hii ni hatua kubwa sana kwenye teknolojia ya kuboresha mafuta,” alisema Mwijage.

Mafuta haya mapya yana uwezo wa kusafisha injini na kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu, kuwezesha matumizi kidogo ya mafuta na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa utokanao na moshi wa vyombo vya moto.

Mafuta ya TOTAL EXCELLIUM yanapatikana katika vituo vyote vya kuuza mafuta vya kampuni ya TOTAL kwa gharama ya bei ya kawaida ya mafuta kwenye soko.

Tarik Moufaddal, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TOTAL nchini anasisitiza, “Kuzinduliwa kwa TOTAL EXCELLIUM, katika soko la Tanzania ni hatua mpya na muhimu kwetu nchini hususani katika kufanikisha dhamira yetu ya kuingiza bidhaa bora za nishati. Tunayo dhamira ya kuwapatia wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, sambamba na huduma bora kupitia mtandao wetu ambao umeenea nchini kote, uzinduzi wa TOTAL EXCELLIUM, unadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi yenye kuleta manufaa katika sekta ya mafuta nchini.”

“TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa teknolojia ya juu ya kisasa ambayo inawezesha kusafisha injini, kuwezesha injini kufanya kazi kwa kipindi kirefu bila kuchoka, matumizi kidogo ya mafuta kuendesha injini, kupunguza uchafuzi wa mazingira utokanao na moshi na ni mazuri kwa matumzi ya aina zote za magari kuanzia madogo mpaka makubwa,” aliongeza Tarik.

“Uzinduzi huu ni moja ya ubunifu mkubwa wa kampuni uliolenga kuhakikisha wateja wetu wanapata bidhaa bora na kuwawezesha matumizi kidogo ya mafuta yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya Excellium. 
"TOTAL EXCELLIUM imetengenezwa kwa ubunifu wa teknolojia za kisasa zenye kuleta ubora. Timu yetu ya wataalamu wa utafiti wamefanikisha kutengeneza mafuta haya kukidhi mahitaji ya wateja wetu wanaotumia magari ya kisasa ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika matunzo ya injini kwa matumizi yao ya kila siku”  Mkurugenzi wa Mtandao wa TOTAL wa Nikesh Mehta.

“Zaidi ya watafiti makini na wataalamu wenye uzoefu mbalimbali wanafanyia kazi suala la kuleta bidhaa za mafuta na vilainishi vya injini na mitambo zenye ubora mkubwa zaidi katika kituo chetu cha utafiti cha Solaize,nchini Ufaransa.Wataalamu hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili kuboresha mafuta ya TOTAL EXCELLIUM. 
"Zaidi ya kanuni za kisayansi 2,300 zimefanyiwa majaribio katika maabara kwa zaidi ya masaa 6,000 na mafuta haya yamefanyiwa majaribio ya awali barabarani kwa zaidi ya masaa 8,500 sawa na kilometa 300,000. 
"Haya yote yanathibitisha uhakika na ubora wa mafuta ya TOTAL EXCELLIUM na yanasafisha injini za magari na kupunguza uharibifu wa mazingira,” anasema Marsha Msuya, Mkurugenzi wa Masuala ya Ndani ya kampuni ya TOTAL.
Credit: Fullshangwe
Read More

Mkuu Wa Majeshi Ahamasisha Vijana Kujiunga Jkt Kupata Stadi Za Kazi Ziwasaidie Kujiajiri


Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.

Jenerali Mabeyo ametoa ushauri huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Juni 07, 2018.

Mabeyo amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya kuajiriwa  .

“Vijana tunaowachukua JKT ni kwa ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili hata kijana akikosa nafasi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza kurudi kijijini akafanya vitu vya maendeleo, mimi nadhani watu wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT lazima aajiriwe,  ipo haja ya kubadili mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo

“Jeshi linachukua vijana elfu ishirini kwa mafunzo, wanaochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama hawazidi vijana 2000 sasa hawa wengine 18,000 wanaenda wapi, kama mawazo yatakuwa ni kwenda JKT ili kuajiriwa hatutafanikiwa lakini kama watakwenda JKT kujifunza stadi za kazi kuwasaidia ili ziwasaidie kujiajiri na kubadili maisha yao tutafanikiwa sana” alisisitiza

Katika hatua nyingine Jenerali Mabeyo ametoa pongezi kwa  juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Simiyu katika mkakati wa Kilimo cha Umwagiliaji ili kuwa na ziada ya chakula cha kutosha.

“Suala la umwagiliaji halikuwepo katika fikra za watu wengi, walio wengi wanategemea mvua na isiponyesha hawalimi na  maisha yanakuwa duni  wanaanza kuilalamikia Serikali, lakini sisi hapa tunayo maji ya Ziwa Victoria, Mkuu wa Mkoa nawapongeza sana kwa juhudi zinazofanywa katika kilimo cha Umwagiliaji, zitasaidia kuwatoa wananchi kwenye ufukara” amesema  Mabeyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema mkoa huo umeweka malengo ya kujitosheleza kwa chakula na kupitia mkakati wa kuwa na mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Mwamanyili wilayani Busega, ambapo amebainisha kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo imeahidi kutoa shilingi bilioni 12kwa ajili ya mradi huo.

“ Lengo letu kama mkoa ni kuifanya wilaya ya Busega kuwa eneo ambalo linafanya vizuri katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa lina maji ya uhakika ya Ziwa Victoria, Benki ya Kilimo wameahidi kutupa shilingi bilioni 12 kwa ajili ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Mwamanyil” alisema Mtaka.

Akizungumzia suala la elimu Mtaka amesema mkoa huo umejipanga kiushindani ambapo madarasa ya mitihani. yatakuwa na makambi ya kitaaluma  ambazo zitawakutanisha wanafunzi kwa ajili ya kupitia maeneo yaliyo magumu ili waweze kujiandaa vema na mitihani ya Kitaifa.

MWISHO
Read More

Alhamisi, 7 Juni 2018

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NCHINI



Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa vituo  vya afya 208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.

Wameyasema hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iliyofika katika kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.

Wananchi hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini  kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas Mkomwa  ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeweza kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, Maabara,  Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti.

Amesema huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya hivyo kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.

“Kwa mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojdhamini mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. Mkomwa.

Naye Richard Mgulumu Diwani wa kata ya Mlali ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa vituo vya afya nchini, hasa kituo cha afya cha Mlali ambapo anasema kuwa awali kituo hicho kilikuwa na wodi chache ambazo zilikuwa hazitoshi kuhudumia wananchi lakini kwa sasa zimeongezeka jambo ambalo litasaidia kuondoa kero za utoaji wa Huduma za afya katika Halamashauri hiyo.

Amesema kuwa Kituo hicho cha afya kimekuwa kikipata wagonjwa wengi kutoka Wilaya ya Kiteto, Wialaya ya Mpwapwa na Malali hivyo kwa ujenzi huo kutasaidia kuwahudumia wananchi maskini ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma bora za afya.

Naye Mganga Mkuu Hospitali ya Jiji la Dodoma Dkt. James Kiologwe ameipongeza Kamati ya Ujenzi ya kituo cha afya cha Mlali kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hicho na kuonyesha uzalendo wa kusaidia jamii.
Aidha timu ya Ufuatiliaji wa ujenzi wa vituo vya afya Jijini Dodoma imekagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Mlali, Chamwino, Hombolo na Makole.
Capt

  1. Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo      kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
  2. Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo.
Majengo ya Upasuaji na wodi ya Wazazi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Mlali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma
Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu      ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo
Read More

Rais Magufuli Atuma Salamu Za Rambirambi Kufuatia Vifo Katika Ajali Mkoani Kigoma


Read More

Jumatano, 6 Juni 2018

PICHA: Basi lagonga treni...10 Wafariki Dunia


Watu 7 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo ambalo linafanya safari zake kutoka Mkoani Kigoma kwenda Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi.

Dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa watu waliofariki, huku idadi ya vifo ikitajwa kuweza kuongezeka, kutokana na majeruhi wengi kuwa kwenye hali mbaya.

Kamanda Otieno amesema kwa sasa jeshi la polisi lipo eneo la tukio likiendelea kuokoa miili na majeruhi wengine, na taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.
Read More

Bavicha: Vifo vya pacha walioungana Maria na Consolata vimeacha funzo


Baraza la Vijana la Chadema, (Bavicha) limesema viongozi hawana budi kushiriki kutoa huduma za afya kwa wananchi badala ya kusubiri pindi wanapofariki.

Akitoa salamu za rambirambi kufuatia vifo vya pacha walioungana, Maria na Consolata leo Juni 6, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrick Ole Sosopi amesema vifo vyao, vimeacha funzo kubwa kwa jamii na Serikali.

Amesema Taifa linapaswa kukubali kuwa kuna tatizo kubwa la huduma za afya na uduni wa mazingira hospitalini.

 “Kila mmoja wetu kwa nafasi yake awaombee wapendwa wetu hawa waliokuwa na vipaji na malengo makubwa katika Taifa, Maria na Consolata Mwakikuti, mbele yetu nyuma yenu, Mungu awape pumziko la amani.

“Bavicha wanatoa pongezi na shukurani kwa Kanisa Katoliki walioweza kuwalea katika kipindi chote cha uhai wao,” amesema Sosopi.
Read More

Hiki Hapa Kinachosababisha Mapacha Kuungana


Hiki Hapa Kinachosababisha Mapacha Kuungana
Imeelezwa kuwa hali ya watoto kuungana hutokea wakati wa mgawanyiko wa seli ingawa si mara zote na chanzo kikuu ni makosa ya taarifa za vinasaba katika mfumo wa uzazi.

Hayo yameelezwa na Dk. Festo Dugange wakati akizungumza na eatv.tv katika mahojiano maalum ambapo amesema kuwa makosa ya taarifa za ‘DNA’ hushindwa kugawanya yai na ndipo hutokea mapacha hao.

"Mbegu ya baba ikikutana na yai la mama ili kutengeneza mtoto, huwa kunatokea mgawanyiko wa seli mara 18 sasa iwapo seli hizo hazikugawanyika na kuachana ikiwa mimba hiyo ni ya watoto pacha basi huzaliwa wakiwa wameungana baadhi ya viungo vyao,” amesema Dk. Dugange.

Ameongeza kuwa  hali hiyo inapotokea wakati mwingine mtoto mmoja hukutwa akiwa amekamilika viungo vyote huku mwenzake akiwa na kasoro kadhaa.
Read More

Kisa Mume, Mwanamke Ajifungulia Polisi


Mwanamke mmoja Amina  Rafael Mbunda (26) mkazi wa Kiswanya,kijiji cha Mgudeni,kata ya mwaya,Tarafa ya Mang'ula wilayani kilombero mkoani Morogoro,anadaiwa kujifungua nje ya kituo cha polisi baada ya kutolewa mahabusu alikokuwa akishikiliwa kwa tuhuma zilizomhusu mumewe aliyedaiwa kuhusika na ununuzi wa kitanda cha wizi.

Mwanamke huyo aliyelazwa kituo cha afya mang'ula alikopelekwa na kulazwa baada ya kujifungua,amedai alikamatwa Juni mosi na polisi,Mwenyekiti wa kitongoji na mwanaume mmoja waliofika nyumbani kwake,saa chache baada ya kuondoka mgambo waliokuwa wakimtafuta mumewe kwa tuhuma za ununuzi wa kitanda cha wizi,ambapo akiwa mahabusu licha ya kulalamika kuumwa uchungu,askari wa zamu alimpuuza hadi alipoona amezidiwa na kumtoa nje alipojifungulia kwenye nyasi bila msaada.

Mganga wa kituo cha afya Mang'ula,aliyetajwa kwa jina moja la Msomba ametafutwa kwa njia ya simu ili afafanue kuhusu afya ya mwanamke huyo na kichanga cha kike kilichozaliwa kikiwa na uzito wa kilo 3.5 kwa mujibu wa kadi yake ya kliniki iliyoonesha pia amejifungua kwa msaada wa ndugu,lakini simu yake iliita bila majibu.
Read More

Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako alivyomwaga machozi msiba Maria na Consolata


Miili ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, imeagwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) kabla ya kuzikwa katika makaburi ya viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo leo Jumatano, Juni 6, 2018.

Maria na Consolata ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa, watazikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili.

Familia za baba na mama wa mapacha hao kutoka Tukuyu, Mbeya na Bukoba, Kagera, waliokuwa walezi wa mapacha hao, masista wa Consolata wa Iringa, na waombolezaji wengine,  wameungana katika kuwasindikiza mapacha hao katika safari yao ya mwisho duniani.
Pia viongozi mbalimbali wa kimkoa na wa kitaifa wameungana na waombolezaji  kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa pacha hao, Maria na Consolata Mwakikuti.

Miongoni mwa waliofika ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Willium. 
Read More

Waziri Ndalichako : “Maria na Consolata ni Mashujaa wa Taifa”


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameongoza waombolezaji  kutoa heshima za mwisho kwa Mapacha walioungana Maria na Consolata mkoani Iringa amabapo alizungumza na waandishi wa habari na kusema mapacha hao  Maria na Consolata  ni  mashujaa wa Taifa  na kwamba wameliacha taifa katika simanzi nzito.

"Mara ya mwisho niliwaona pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa mahututi, inaniumiza mno lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe," amesema.

Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu waliokuwa wakipigania elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo.

Read More