Miili
ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki dunia Jumamosi
iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, imeagwa katika viwanja
vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) kabla ya kuzikwa katika makaburi ya
viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo leo Jumatano, Juni 6,
2018.
Maria na Consolata ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa, watazikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili.
Familia
za baba na mama wa mapacha hao kutoka Tukuyu, Mbeya na Bukoba, Kagera,
waliokuwa walezi wa mapacha hao, masista wa Consolata wa Iringa, na
waombolezaji wengine, wameungana katika kuwasindikiza mapacha hao
katika safari yao ya mwisho duniani.
Pia
viongozi mbalimbali wa kimkoa na wa kitaifa wameungana na waombolezaji
kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa pacha hao, Maria na Consolata
Mwakikuti.
Miongoni mwa waliofika ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Willium.
Miongoni mwa waliofika ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Willium.
0 comments:
Chapisha Maoni