Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema amesema msanii wa Bongo
Flava anayemfuatilia kwa sana ni Diamond Platnumz.
Ameeleza sababu ya kumfuatilia muimbaji huyo ni kutokana na kujituma kwake na muziki wake unavutia.
“Namfuatilia
sana Diamond, ni kijana mdogo, muimbaji mahiri, yaani Diamond asaidiwe
naona hatima yake katika maisha yake na nchi yetu atatufikisha mahali
pazuri. Kwa muziki wake unakosha roho, hata sisi wazee, mimi naridhika
sana,” Mrema ameiambia Times FM.
Katika
hatua nyingine ametoa wito kwa serikali kuwa karibu zaidi na wasanii,
hata hivyo amesema anaziona jitihada za Waziri wa Habari, Utamaduni
Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe za kukutana na wasanii kila
mara hasa pale wanapopata matatizo na kuwasaidia.
0 comments:
Chapisha Maoni