Polisi
Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata Mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumkaba
shingoni mtoto wake wa miaka 5 na kisha kumtupa katika mto Rutui.
Kwa
mujibu wa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa Mwanamke huyo mwenye miaka
23 ambaye anaishi peke yake, baada ya kutenda tukio hilo alimtupa mwanae
kwenye mto na kukaa kimya akiamini kuwa maiti ya mtoto wake
itachukuliwa na maji na kupelekewa sehemu isiyojulikana.
Duru
za kuaminika zinasema kuwa ndugu wa mtuhumiwa huyo walianza kumuulizia
mtoto na mtuhumiwa akawa anawajibu kuwa na yeye anashangaa kutoweka
kwa mwanae.
Aidha
mwili wa mtoto huyo ulionekana ukielea katika mto Rutui asubuhi ya June
9 na ndipo wakazi wa eneo hilo ikiwemo mtuhumiwa waliwaita Polisi na
kuutoa mwili wa mtoto huyo kisha wakamkamata mtuhumiwa.
Kwa
mujibu wa Polisi wa kituo cha Kirinyaga Yaya Chome amesema kuwa
mwanamke huyo amefunguliwa mashitaka ya kusudio la kutaka kuua katika
mahakama ya Kerugoya.
Chanzo cha mama huyo kutenda tukio hilo la kinyama bado hakijawekwa wazi.
0 comments:
Chapisha Maoni