test
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KIMATAIFA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KIMATAIFA. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 14 Juni 2018

Michuano ya Kombe la Dunia Kuanza Leo Urusi


Related image
Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa ya mwaka 2018 inaanza leo nchini Urusi ambapo Urusi watacheza dhidi ya Saudi Arabia baada ya kufanyika kwa sherehe ya ufunguzi katika uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow.

Mechi hiyo itaanza saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki.

Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.

Fainali itachezwa 15 Julai.

Fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800.

Kutokana na hili, kutakuwa na tofauti kubwa katika wakati mechi zinachezwa.

Ujerumani, waliowashinda Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2014, wanapania kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1962.
Read More

Jumatatu, 4 Juni 2018

Chris Brown Aanza Kujirudisha kwa Rihanna


Chris Brown Aanza Kujirudisha kwa Rihanna
Ukisema cha nini wenzako wanasema watakipata lini. Chris Brown ameanza kuwasha taa ya kijani kumfukuzia upya Rihanna.

Chris amemfollow Rihanna kwenye Instagram ikiwa ni muda mfupi baada ya taarifa za mrembo huyo kuachana na mpenzi wake, Hassan Jameel.

Hatua hiyo ya Chris imeonekana kama bado anamfukuzia mrembo huyo ambaye aliwahi kummiliki mwaka 2007 na walimwagana 2009.

Rihanna na Hassan ambaye ni tajiri wa Saudi Arabia wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tangu Juni mwkaa jana, ila imeripotiwa kuwa kwa sasa wameachana na Rihanna ndiye aliyevunja mahusiano hayo.
Read More

Cristiano Ronaldo Ataka Kurudi Manchester United Kuungana na Mourinho.


Cristiano Ronaldo Ataka Kurudi Manchester United Kuungana na Mourinho.
KOCHA wa zamani wa Real Madrid na England, Fabio Capello amefichua kuwa Cristiano Ronaldo anataka kurudi Manchester United ili aungane na mreno mwenzake Jose Mourinho.

Kitendo cha Zinedine Zidane kuachia ngazi kuinoa Real Madrid kimezua hali ya taharuki ndani ya klabu hiyo, ambapo sasa mustakabali wa nyota wawili wa timu hiyo Ronaldo na Gareth Bale umekuwa suala gumu.

Nyota hao wawili kwa sasa wanahusishwa na kujiunga na Manchester United kwa ajili ya msimu ujao.

Ronaldo alizua mtafaruku baada ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, ambapo aliwashukuru mashabiki wa Real kwa ushirikiano waliompa kipindi alichokuwa katika timu hiyo akiashiria kama anawaaga.

Kwa miaka mwili sasa kumekuwa kuna uvumi kuwa staa huyo anataka kuihama klabu hiyo akilalamikia ushirikiano finyu kutoka kwa uongozi.

Capello anasema kutokana na Ronaldo na Mourinho kufanya kazi pamoja Real Madrid kuanzia 2010 na 2013 walijenga uelewano mkubwa ukizingatia wote wanatoka Ureno.

“Cristiano anataka kurudi Manchester United ili akafanye kazi na Mourinho,” alisema Capello katika mahojiano na televisheni ya Sky Sport 24.
“Ninadhani hatimaye ataondoka Real Madrid na kurudi zake Manchester United alipotengeneza jina lake,” aliongeza Capello.

Hata hivyo, uamuzi juu ya mustakabali wa Bale na Ronaldo utawekwa bayana baada ya Real Madrid kupata kocha mpya.

Nyota hao wawili walianza kutamba kwenye Ligi Kuu England, ambapo Ronaldo alichezea Manchester United mwaka 2003 hadi 2009 wakati Bale alikuwa Tottenham tangu 2007-2013.

Real Madrid inaendelea na mchakato wa kupata kocha mpya huku kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino akipewa nafasi kubwa ya kukabidhiwa mikoba ya Zidane.
Read More

Volkano Yasabisha Vifo vya Watu Saba Guatemala


Volkano yasabisha vifo vya watu saba Guatemala
Serikali ya Guatemala imesema kuwa majivu ya volkano kutoka mlima mmoja unaoendelea kulipuka, yamesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine ishirini.

Shirika la kukabiliana na majanga nchini Guatemala limesema kuwa mlima Fuego ulilipuka siku ya jumapili, huku majivu hayo yakirushwa hadi kijiji cha El Rodeo na kusababisha uharibifu mkubwa wa makaazi ya watu.



Wahamiaji takribani 35 wapoteza maisha baada ya Boti kupinduka Tunisia
Pacha walioungana Tanzania waliowagusa wengi wafariki dunia
Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhali imetolewa.

Hata hivyo ya watu hao waliokufa kati yao watatu ni watoto.

Mlima Fuego ukifuka moshi baada ya Volkano kulipuka
Read More

Rais wa Syria Bashar al- Assad kutembelea Korea Kaskazini


Rais wa Syria, Bashar al-Assad anapanga kutembelea nchini Korea Kaskazini,Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeeleza.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuhodhi ziara ya Kiongozi wa nchi tangu alipoingia marakani mwaka 2011

Hivi karibuni amekuwa na shughuli nyingi za kidiplomasia, kukutana na Rais wa China mwezi Mei na anatarajiwa kuhudhuria mkutano na Donald Trump mwezi huu

Syria, mshirika wa Korea Kaskazini, haijasema lolote kuhusu mpango huo unaoripotiwa.

Nchi hizi mbili zimekuwa zikishutumiwa kushirikiana katika mapngo wa kutumia silaha za kemikali.Lakini nchi hizi zimekana shutuma hizo

Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa wazina vyombo vya Korea Kaskazini.

Vilimnukuu bwana Assad siku ya Jumatano akisema ''ninakwenda kutembelea Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong-un."

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili ulianza mwaka 1966 na kutuma vikosi na silaha wakati wa vita vya Arab na Israeli mwezi Oktoba mwaka 1973

Ripoti ya Umoja wa mataifa ilivuja mwezi Februari ikishutumu Korea Kaskazini kwa kufanya safari za meli takriban 40 kuelekea Syria kati ya mwaka 2012 na 2017, meli zinazodaiwa kubeba acid, mipira na bidhaa nyingine zinazodaiwa kuw zinaweza kutengeneza silaha za kemikali.

Assad ameshutumiwa kutumia silaha za kemikali wakati wa vita vya miaka saba nchini humo lakini amekana kuwa na kemikali hizo.
Credit: BBC
Read More

Ijumaa, 1 Juni 2018

Kinyume na ilivyotegemewa na Wengi...Kocha Zidane Ajiuzulu Real Madrid


HISPANIA: Kocha wa Real Madrid, Mfaransa Zinedine Zidane leo Mei 31, 2018 ametangaza kujiuzulu kufundisha klabu hiyo kwa msimu ujao ikiwa ni siku tano baada ya kuipa ubingwa wa UEFA Champions League mara ya 3 mfululizo.

Zidane anaondoka klabuni hapo kwa heshima baada ya kuitumikia kwa miaka miwili. Mfaransa huyo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo.

Mkongwe huyo wa soka mwenye miaka 45, baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa ilikuwa inatabiriwa angeongezewa mkataba hadi mwaka 2020. Hata hivyo awali kulikuwa na presha kubwa kutoka uongozi wa Madrid kutokana na kutofanya vyema kwenye La Liga msimu huu ulioisha.

Makocha Arsene Wenger na Antonio Conte ni miongoni mwa wanaotajwa kumrithi Zidane, huku Conte akipewa nafasi kubwa Zaidi.

Zidane alimrithi kocha Rafael Banitez Januari 2016 na msimu huo huo aliipa taji la Ligi ya Mabingwa timu hiyo.

Zidane ameitumikia Madrid tangu (2016-18)
UEFA Champions League🏆🏆🏆
UEFA Super Cup🏆🏆
Club World Cup🏆🏆
Spanish Super Cup🏆
Liga🏆
Read More

Mo Salah kukosa dakika 90 tu Urusi





STAA wa Misri, Mohamed Salah, atakosa mchezo mmoja tu wa Kombe la Dunia baada ya hapo atakuwa fiti. Salah aliumia bega kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid baada ya kuumizwa na Sergio Ramos.
Hata hivyo, kulikuwa na hofu kuwa staa huyo atashindwa kucheza fainali hizo lakini sasa imefahamika kuwa atakwenda na kukosa mchezo mmoja tu kwa kuwa kuanzia leo atakuwa nje kwa wiki tatu tu.
Shirikisho la Soka la Misri, limesema kuwa madaktari wanapa-mbana kuhakikisha kuwa mchezaji huyo anakuwa fiti.
Salah anaendelea na matibabu nchini Hispania na ataungana na wenzake hivi karibuni kabla ya safari ya kwenda Urusi kwenye fainali hizo ambazo zitaanza Juni 14.
“Mohamed Salah atakuwa nje kwa wiki tatu, kutokana na jeraha ambalo alilipata kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Ukraine.
“Atakuwa kwenye Kombe la Dunia, lakini atakosa mchezo dhidi ya Uruguay, ingawa bado juhudi zinaendelea kuhakikisha anakuwa fiti.
“Wakati huu anaendelea na matibabu, atakuwa nje ya kambi ya mazoezi na wenzake,” ilisema taarifa kutoka kwenye shirikisho hilo.
Salah ndiye staa wa Misri baada ya kumaliza msimu akiwa na mabao 44, kwenye klabu yake ya Liverpool na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu England. Misri wapo kundi A, wakiwa na wenyeji Urusi, Saudi Arabia na Uruguay.
Read More

Alhamisi, 31 Mei 2018

Mo Salah kushiriki katika kombe la dunia Urusi


Image result for Mo SalahMshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah ataweza kushiriki katika michuano ya kombe la dunia , tafa lake limetangaza.
Daktari wa timu ya taifa hilo amesema kuwa matibabu ya kiungo huyo wa mashambulizi hayatachukua zaidi ya wiki tatu huku taifa lake likitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya 

Uruguay mnamo tarehe 15 mwezi Juni.
Salah, 25, alikutana na daktari huyo pamoja na rais wa shirikisho la soka nchini Misri Hany Abu Rida nchini Uhispania siku ya Jumatano.

Shirikisho hilo baadaye lilituma ujumbe wa Twitter likisema: Baada ya kukutana na Abu Rida pamoja na daktari wa timu ya taifa nchini Uhispania leo, Shirikisho la soka linathibitisha kuwa Salah atashiriki katika kombe la dunia, Mungu akipenda.
Awali mshambuliaji huyo hakuwa katika hali ya kuweza kuzungumza zaidi na wanahabari wakati alipowasili nchini Uhispania kwa matibabu ya bega lake.
Mshamuliaji huyo aliyevunja rekodi za ufungaji wa mabao katika klabu yake ya Liverpool alipata jeraha katika mechi ya fainali ya vilabu bingwa ambapo timu yake ililazwa 3-1 na hatimaye mabingwa wa kombe hilo Real Madrid wiki moja iliopita.

Salah alipata jeraha hilo alipokuwa aking'ang'ania mpira na beki wa Real Madrid Sergio Ramos.
Alilazimika kutolewa huku kukiwa na hofu ya iwapo ataweza kuichezea Misri katika fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwezi ujao.

Shirikisho la soka nchini Misri FA lilithibitisha siku ya Jumatatu kwamba Salah ataelekea Valencia kwa matibabu ambapo ataandamana na maafisa wa matibabu wa klabu ya Liverpool.

Salah aliwasili mjini humo siku ya Jumanne alfajiri ambapo mwanahabari mmoja wa Uhispania alijaribu kutafuta majibu kuhusu hali yake ,na iwapo ataweza kusafiri kuelekea Urusi na iwapo anamlaumu Ramos kwa jeraha hilo.
Read More

Jumatano, 30 Mei 2018

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu aapa kujibu mashambulizi dhidi ya Wanamgambo wa Kipalestina


Majeshi ya Israel yameushambulia Ukanda wa Gaza baada ya wanamgambo wa Kipalestina kufanya mashambulizi mapya ya makombora kuelekea kusini mwa Israel.

Jeshi la Israeli limefanya mashambulizi katika Ukanda wa Gaza baada ya wanamgambo hao wa Kipalestina kurusha takriban makombora 28 ndani ya Israeli, ambayo yaliufyatua mfumo wa kinga dhidi ya silaha wa Israel wa Iron Dome.

Kundi la Hamas linalotawala katika Ukanda wa Gaza, na washirika wake wa kundi dogo la wapiganaji la Islamic Jihad wamethibitisha kwamba kambi zao za kijeshi zimeshambuliwa kwa mabomu ingawa hakuna watu walioripotiwa kujeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya Israel.

Mashambulizi ya  kutoka Gaza ndiyo ya kwanza kutokea tangu kuanza wimbi jipya la maandamano tarehe 30 Machi. 
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amelaani mashambulizi hayo kuilenga jamii ya Waisraeli kutokea kwenye Ukanda Gaza na amewalaumu wanamgambo wa Hamas kwa kuchochea vurugu na hali ya wasiwasi.
 
Msemaji wa jeshi la Israel Jonathan Conricus amewaambia waandishi wa habari kwamba mashambulizi hayo ya roketi na mizinga ni makubwa ukilinganisha na vita vya mwaka 2014 hali kadhalika lilivyokuwa jibu la Israeli. 
Msemaji huyo wa jeshi la Israel ameelezea kwamba wameyashambulia malengo zaidi ya 30 ya kijeshi ya mashirika ya kigaidi.

Wakati huo huo mashua iliyokuwa na wanaharakati 20 wa Kipalestina waliokuwa wakijaribu kuvunja marufuku ya miaka 11 katika pwani ya Gaza ilizuiwa na vikosi vya Israeli kwa mujibu wa mratibu wa maandamano hayo.
 
Israeli imesema kutokana na sababu za usalama inazizuia boti zote kutoka Gaza kuvuka eneo la uvuvi lililowekewa marufuku kwa umbali wa kilomita kadhaa. 
Hapo awali wavuvi wa Gaza walipigwa risasi na majeshi ya Israel kwa sababu ya kuivunja amri hiyo. Mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo, Adham Abu Selmeya, amesema manowari za kijeshi nne za Israel zilitumika kuyazuia maandamano ya mashua maili tisa kutoka pwani.

Mvutano katika Ukanda wa Gaza umefikia kiwango cha juu katika wiki za hivi karibuni. Wapalestina zaidi ya 100 waliuawa na majeshi ya Israeli wakati wa maandamano makubwa yaliyofanyika mpakani mnamo mwezi Machi.

Eneo la Ukanda wa gaza linakumbwa na hali mbaya ya kiuchumi, kutokana na uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na vita vilivyotokea mara tatu kati ya Wanamgambo wa Hamas huko Gaza na Israeli na  pia kuna ukosefu mkubwa wa bidhaa.
Credit: DW
Read More

Burundi Yachikia Baada ya Kupewa Zawadi ya PUNDA Na Ufarasa, Yadai Hizo ni Dharau


Burundi imeonesha kukasirishwa na kitendo cha Serikali ya Ufaransa kupitia taasisi yake kutoa punda kama zawadi yake kwa wanakijiji wa Gitega nchini humo.

Punda hao walionunuliwa nchini Tanzania waliwasilishwa kwa wanakijiji hao kama sehemu ya mradi wa kuwasaidia wanawake na watoto kusafirisha mazao ya kilimo, maji pamoja na kuni.

Hata hivyo, mshauri wa Rais ameitaja zawadi hiyo kama matusi kwa taifa hilo la Afrika Mashariki, akisema kuwa imebeba ujumbe mbaya kutoka Ufaransa.

Gabby Bugaga, msemaji wa seneti ya Rais pia aliandika ujumbe kwenye Twitter akieleza kuwa, “Ufaransa wanatuchukua kwa punda”.

“Kuweni wakweli, punda ni ishara ya ubora au ubovu,” aliongeza kwenye tweet yake.

Jumapili iliyopita, Waziri wa kilimo wa Burundi, Deo Guide Rurema aliwataka watendaji kuhakikisha wanarudisha haraka punda wote waliowasilishwa kama zawadi kwa wanakijiji, akiongeza kuwa usambazaji wake haukufuata taratibu.

Alhamisi iliyopita, mradi huo ulizinduliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Burundi, Laurent Delahousse ambaye aliusifia.

Mwanadiplomasia wa Ulaya ambaye alizungumza na shirika la habari la AFP kwa masharti ya kutotajwa jina alisema kuwa uamuzi huo wa Burundi ni kulipiza kisasi kutokana na kauli ya Ufaransa ya hivi karibuni ya kukosoa uendeshwa na matokeo ya kura za maoni ambayo yanampa nafasi Rais Pierre Nkurunziza kuongeza mihula miwili itakayokamilika mwaka 2034.
Read More

Aliyeachiwa kwa muda gerezani afyatua risasi na kuua askari, raia


Mwanaume mmoja mwenye silaha amefyatua hovyo risasi na kuwaua askari wawilio wa kike wa jeshi la polisi na raia mmoja Mashariki mwa jiji la Liege nchini Ubelgiji.

Katika tukio hilo lililofanyika jana, mtu huyo pia ameripotiwa kumteka mfanyakazi wa usafi na kumtumia kama kinga, kabla ya kuuawa na askari wa jeshi la polisi waliofika katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la nchini humo la RTBF, mshambuliaji huyo aliachiwa hivi karibuni kutoka jela kuwa chini ya kipindi cha matazamio alipokuwa akitumikia kifungo cha makosa ya dawa za kulevya.

Ingawa bado haijafahamika chanzo cha uamuzi wa mshambuliaji huyo kufanya tukio la mauaji, Serikali ya Ubelgiji imesema kuwa inalichukulia tukio hilo kama tukio la kigaidi na kwamba huenda mtu huyo alifundishwa ugaidi alipokuwa amefungwa jela.
 
Meya wa Liege, Willy Demeyer amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji alipofanya mkutano na waandishi wa habari. Meya huyo amesema kuwa watatoa msaada wa kisaikolojia na vitendo kwa familia za marehemu.

Muendesha mashtaka wa Serikali amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya asubuhi karibu na mgahawa katikati ya jiji hilo. Amesema kuwa mshambuliaji aliwanyemelea askari, akamchoma kisu askari mmoja na kumnyang’anya bunduni kabla ya kuanza kufyatua risasi.
Read More

Wanamgambo wa Gaza waishambulia Israel


Wanamgambo wa Kipalestina huko Gaza wamevurumisha makombora kadhaa kusini mwa Israel jana. Hata hivyo mashambulizi hayo hayakusababisha majeraha, lakini yameongeza hali ya wasiwasi katika eneo la mpakani.

Taarifa ya jeshi la Israel ilisema makombora 25 yamevurumishwa kuelekea maeneo kadhaa nchini Israel, huku mengi yakizuiwa na mfumo wa kuzuia makombora wa Iron Dome. Polisi walisema makombora kadhaa yameanguka katika maeneo ya wazi upande wa Israel, lakini hakuna ripoti zozote za majeruhi zilizotolewa.

Jeshi lilisema makombora mengine mawili yalifyatuliwa kutokea Gaza baada ya mfululizo wa kwanza wa makombora, moja limelipuka karibu na jengo la shule ya chekechea lakini inaaminiwa hakukuwa na mtoto yeyote ndani ya jengo hilo wakati wa tukio.

Duru za usalama za Palestina zilisema vifaru vya Israel vimeyashambulia maeneo ya kufuatilia matukio ya makundi ya Hamas na Islamic Jihad karibu na mpakani. Msemaji wa jeshi la Israel alisema hana taarifa kuhusu hujuma hiyo.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliapa kuchukua hatua kali. "Israel huchukulia kwa uzito mkubwa mashambulizi dhidi yake na jamii zake yanayofanywa na Hamas na Islamic Jihad kutokea Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel litajibu mashambulizi haya kwa nguvu," alisema Netanyahu wakati wa mkutano kaskazini mwa Israel.
Read More

Jumanne, 29 Mei 2018

Robert Mugabe Akishindwa Kutimiza Sharti Hili Atakamatwa na Polisi


Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kwa mara ya pili ameshindwa kufika mbele ya Kamati ya Uchunguzi ya Mapato ya Almasi ya Bunge la nchi hiyo.

Mugabe anahitajika kuhojiwa na kamati kuhusu madai ya upotevu wa mapato ya almasi kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 15 katika kipindi cha utawala wake.

Mugabe alitakiwa kwa mara ya kwanza kutokea mbele ya kamati May 23, 2018 saa 3 asubuhi na kutotokea kwake kulidhaniwa kuwa ni sababu ya uzee hivyo alishindwa kufika muda wa asubuhi.

Kwa mara ya pili Mugabe alitakiwa kufika May 28, 2018 saa 7 mchana lakini pia ameshindwa kufika hivyo kama sheria inavyosema ataitwa mara ya 3 kabla vyombo vya dola havijapewa kazi ya kumfikisha Bungeni kwa nguvu.

Rais huyo aliyeongoza kwa muda mrefu hadi alipotolewa madarakani Novemba mwaka 2017, ametakiwa kufika Bungeni hapo tarehe June 11, 2018 bila kukosa.
Read More

Mahakama Moshi yapokea hoja tisa kesi ya Bilionea Msuya


Mawakili  wa utetezi katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa madini ya tanzanite ‘Bilionea’ Erasto Msuya (43), jana walitumia saa nne na nusu kuwasilisha hoja tisa za majumuisho kwa lengo la kuonyesha mahakama kuwa wateja wao hawana hatia.

Hoja hizo zilizowasilishwa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi chini ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza shauri hilo namba 12 la mwaka 2014, zilijikita zaidi kuhoji utaratibu mzima wa ukamataji washtakiwa.

Jaji Maghimbi alianza kusikiliza hoja za upande wa utetezi jana saa 4:08 asubuhi hadi saa 7:32 mchana alipoahirisha kwa muda usikilizaji wake hadi saa 7:45.

Washtakiwa walioonekana wana kesi ya kujibu ni mshtakiwa wa kwanza Sharif Athuman (35), ambaye ni mfanyabiashara wa madini na mchimbaji mdogo, mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, mshtakiwa wa pili Shaibu Saidi maarufu kama Mredii (42), mkazi wa Songambele, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara na mshtakiwa wa tatu Mussa Mangu (34), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu.

Wengine ni mshtakiwa wa tano Kihundwa, mkazi wa Lawate, Wilaya ya Siha, mshtakiwa wa sita Sadiki Jabir a.k.a Msudani (36), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata, Wilaya ya Hai, na mshtakiwa wa saba Alli Musa maarufu Majeshi, mkazi wa Babati, mkoani Manyara.

Aliyekuwa mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo iliyobaki na washtakiwa sita, Jalila Said (32) mkazi wa Babati aliachiwa huru Mei 14 baada ya Jaji Maghimbi kuona ushahidi uliotolewa dhidi yake haumgusi kiasi cha kufanya awe na kesi ya kujibu.

Msuya, aliuawa kwa kupigwa risasi 22, Agosti 7, 2013, majira ya saa 6:30 mchana katika eneo la Mijohoroni, kando ya barabara kuu ya Arusha-Moshi, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Mawasilisho ya uchambuzi wa hoja hizo yaliyofanywa na Wakili Majura Magafu katika waraka wenye kurasa 34, ulijikita zaidi kwenye uchambuzi wa mkanganyiko wa tarehe halisi za ukamataji wa watuhumiwa, utata wa tarehe za kupatikana vielelezo muhimu vya ushahidi kama bunduki aina ya SMG, pikipiki mbili zinazodaiwa kutumiwa na wauaji, maelezo yanayodaiwa ni ya kukiri kosa na ripoti ya DNA.

Hoja nyingine ni mateso ya washtakiwa, umiliki wa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Motii Mongululu inayodaiwa kutumika kumvuta marehemu kwenda eneo la tukio na kama ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka ni ushahidi wa moja kwa moja au ni wa ushahidi wa kimazingira.

Akichambua hoja hizo, Wakili Magafu alidai hakuna ubishi kwamba Msuya alikufa kifo ambacho si cha kawaida cha kupigwa risasi na kuvuja damu nyingi, lakini pia hakuna ubishi kwamba shahidi pekee aliyeshuhudia mauaji hayo ni kijana wa miaka 19, Noel Thomas, mkazi wa Kijiji cha Ormelili, Wilaya ya Siha aliyekuwa akichunga mifugo lakini hakuweza kumtambua aliyefyatua risasi kumuua.

“Mheshimiwa Jaji (Maghimbi), kumekuwa na utata kuhusu ukamataji wa watuhumiwa, washtakiwa waliopo mbele yako wanasema tarehe zilizotajwa katika maelezo yao sizo tarehe walizokamatwa," alidai wakili Magafu na kueleza zaidi:

"Swali la kujiuliza ni hili je, hiyo caution statement (maelezo ya onyo) iliyokuwa admitted (pokelewa) hapa mahakamani na kusajiliwa kama Exhibit P.II (kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka namba II) kina sifa ya kuitwa confession statement (maelezo ya kukiri kosa)?

"Ni lazima confession statement iweze kukutia kwanza wewe hatiani na vile vile tunasema haiwezi kutumika kuwatia wenzako hatiani. Hakuna ushahidi uliotolewa hapa mahakamani ukionyesha Musa Mangu alihusika kununua na kuchonga laini za simu zilizotumika katika mauaji hayo zaidi ya maelezo ya wapelelezi.

"Mtu pekee ambaye angeweza kuisaidia mahakama na hakuletwa mahakamani kutoa ushahidi wake ni Adam Leyani.”

Wakili Magafu aliendelea kudai kwamba mshtakiwa wa kwanza, Mussa Mangu anadaiwa alikamatwa kati ya Agosti 11 na 13, 2013 na mkanganyiko huo umeletwa na shahidi wa 27 wa upande wa Jamhuri ambaye anakinzana na shahidi wa 18 na wote ni maofisa wa polisi.

Aidha, aliendelea kudai kuwa katika ukamataji wa bunduki upande wa mashtaka umedai kuwa ilikamatwa Septemba 11, 2013 lakini ushahidi huo huo unaonyesha kwamba watuhumiwa walikamatwa Septemba 13, 2013.

“Swali tunalojiuliza na ambalo mahakama inapaswa ilizingatie ni kwamba ni nani kati ya washtakiwa waliopo mbele ya mahakama alitumia bunduki hiyo (SMG) kumfyatulia risasi marehemu Msuya? Ushahidi huo haupo," alidai Wakili Magafu.

"We submit the gun was planted by the police (tunasema bunduki ilibambikwa na polisi) kwa sababu ilipatikana kabla ya watuhumiwa kukamatwa. Kukosekana kwa chronological events (mtiririko wa matukio) kunaacha utata.”

Aidha, wakili huyo aliyekuwa akiwasilisha hoja hizo kwa niaba ya wenzake watatu alidai kwamba hakuna ushahidi wa kuonyesha kwamba miongoni mwa watuhumiwa hao alikuwapo anayemiliki pikipiki aina ya King Lion na kutumia SMG hiyo kumuua Bilionea Msuya na kwamba ni jukumu la upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka.

Wakili Magafu aliendelea kudai kuwa kwa mshtakiwa wa pili Athuman ushahidi wa Jamhuri una mkanganyiko kwa vile shahidi wa 27, Mkaguzi wa Polisi Damian Chilumba alidai alikamatwa Agosti 12, 2013 lakini shahidi wa tisa, Mkaguzi wa Polisi Samuel Maimu akaieleza mahakama kwamba alikamatwa Agosti 13 mwaka huo.

Zaidi aliendelea kudai kwamba kwa 'Mredii’ ushahidi wa shahidi wa upande wa mashtaka alidai mahakamani hapo kwamba Mredii alikamatwa Agosti 16,2013 lakini shahidi wa utetezi ambaye ni yeye Mredii alidai kwamba hakukamatwa na polisi isipokuwa aliitwa kwa wito na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani na alitii na kwenda siku ya Agosti 17, 2013.

Kuhusu ushahidi wa uchunguzi wa DNA, Wakili Magafu alidai kwamba ushahidi wa shahidi wa 25 wa upande wa mashtaka, Gloria Omari (55) aliyekuwa akifanya kazi za kemia na utafiti kwenye Maabara ya Idara ya Sayansi ya Jinai ya Vinasaba katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali mwaka 2013, ushahidi wake hauungi mkono ushahidi wa shahidi wa 26, Kaijunga Brassy (35) ambaye alikuwa Mkemia kutoka Makao Makuu ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini.

Wakati anahitimisha uwasilisha hoja hizo, Wakili Magafu aliieleza mahakama hiyo kwamba hakuna ushahidi wa moja kwa moja katika kesi hiyo na kwamba mahakama imebaki na ushahidi mmoja ambao ni wa kimazingira.

"Mheshimiwa Jaji na waungwana wazee wa mahakama ili ushahidi wa circumstantial uweze kutumika ni matakwa ya sheria kwamba mnyororo wa ushahidi haupaswi kukatika," alidai.

"Ushahidi wa prosecution (Jamhuri) unakatika mno na ushahidi huo wa kimazingira wanaojaribu kuuleta mnyororo wake umekatika. Mahakama inastahili iwaone washtakiwa hawana hatia, prosecution wameshindwa kuthibitisha kesi yao na washtakiwa waachiwe huru."

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo ambayo ni gumzo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, unaongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Abdala Chavula, akisaidiwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Omari Kibwana na Wakili wa Serikali, Kassim Nassir.

Mawakili wanaounda jopo la utetezi katika kesi hiyo ni Hudson Ndusyepo anayemtetea mshtakiwa wa kwanza, Magafu anayemtetea mshtakiwa wa pili na wa tano, Emmanuel Safari anayemtetea mshtakiwa wa tatu na John Lundu anayemtetea mshtakiwa wa nne, sita na saba.
Read More

Jumatatu, 28 Mei 2018

Real Madrid walivyosherehekea na kombe la UEFA Hispania, Ronaldo aimbiwa wimbo na mashabiki (picha)



Mabingwa wapya barani Ulaya, Real Madrid usiku wa kuamkia leo Mei 28 wamefanya sherehe kubwa ya kuwaonesha mashabiki wao Kombe kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid nchini Hispania.
Kabla ya Sherehe hizo jana mchana wabingwa hao walitembeza kombe la UEFA kwenye viunga vya jiji la Madrid wakiwa kwenye gari maalumu la wazi.



Kilichosisimua zaidi wakati wa sherehe hizo ni pale mshambuliaji wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo aliposimama na kutoa hotuba fupi ambayo hata kabla ya kumaliza hotuba hiyo wachezaji wenzake na mashabiki walimkatiza kwa kuimba wimbo uliokuwa unasikika kwa maneno ya “Ronaldo Stay, Ronaldo Stay”. Tazama video na picha za matukio yote.



Read More

Kijana Shujaa wa Nchini Mali Aliyemuokoa Mtoto Ghorofani Akutana na Rais, Apewa Uraia na Kazi Serikalini


Kijana Shujaa  wa Nchini Mali Aliyemuokoa Mtoto Ghorofani Akutana na Rais, Apewa Uraia na Kazi Serikalin
Kijana raia wa nchini Mali, Mamoudou Gassam (22) ambaye Jumamosi iliyopita amefanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo ambaye alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nzito.



Mamoudou amekutana na Rais Macron mapema Jumatatu hii kwenye Ikulu ya Elysee Palace kwa ajili ya kufanya mazungumzo pamoja na kupongezwa kwa msaada alioutoa.

Rais Macron amempatia cheti cha Uraia wa Ufaransa kijana huyo ambaye alihamia nchini hapo kwa njia zisizokuwa za kihalali takribani miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kutafuta maisha.


Kupitia mtandao wa Twitter Rais Macron ameweka picha akiwa Ikulu na kijana Mamoudou na kuandika, “With Mr. GASSAMA who saved Saturday the life of a child climbing 4 floors with bare hands. I announced to him that in recognition of this heroic act he would be regularized as soon as possible, and that the brigade of the firemen of Paris was ready to receive it.”
Read More

Korea Kaskazini Yasisitiza Ipo Tayari Kwa Mazungumzo na Marekani


Ni nia ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuwa mkutano kati yake na Rais wa Marekani Donald Trump uendelee, imeeleza taarifa ya vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.
Read More

Jumapili, 27 Mei 2018

Mo Salah atacheza World Cup? Daktari wa timu atoa neno hili.


Mtanange wa yule Bingwa wa Ulaya umekamilika. Real Madrid wameshinda taji lao la tatu mfululizo kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja. Golikipa wa Liverpool Karius akisababisha uzembe ulioigharimu timu hao baada ya kurusha mpira kimakosa na ukagomga Benzema aliyegfunga bao la kwanza kabla ya Mane kusawazisha. unga magoli mawili. Bale alitokea benchi na kufunga mabao mawili.
Read More

Alhamisi, 24 Mei 2018

Wanawake 40 Kunyongwa Iraq


Serikali inatarajia kuwanyonga wachumba 40 wa wanamgambo wa Dola ya Kiislamu (IS) kulipiza kisasi kwa wapiganaji hao wa jihadi kuikalia kwa miaka mitatu ardhi ya Iraq wakati wa mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kuuawa kikatili.
Read More

Facebook Yaendelea Kuomba Msamaha


Mkurugenzi wa Facebook Mark Zuckerberg ameomba msamaha kwenye Bunge la Ulaya kutokana na madhara yaliyosababishwa na kuvuja kwa data za watumiaji wa mtandao huo na pia kwa kushindwa kupambana na habari za uongo/ feki.
Read More