test
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UDAKU. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UDAKU. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 12 Juni 2018

Je Wajua Kuwa Unapofanya Mapenzi na Mtu Unaweka Agano la Damu?


Unapohusiana na mtu kimapenzi unafanya naye agano la damu. Agano hilo maana yake ni kwamba wewe unakubaliana na kufungamana na sifa na tabia pamoja na vifungo vingine vyote kama vile laana, mizimu, matatizo na majanga mbalimbali yanayomhusu huyo uliyefanya naye mapenzi, kadhalika na yeye anafungamana na wewe katika mambo hayo. Agano la namna hiyo humtaka aliyeingia katika hayo mapatano kukubaliana nayo "consistently". Iwapo mhusika hatatii au ataenda kinyume na agano, ndipo agano hilo "hutrigger malice" na kusababisha kutokuelewana, vurumai, kutokupendana na hata kuuana katika mahusiano na mara nyingi kupelekea kuachana!

Kimsingi, unapojamiana na mtu unakubaliana naye kuchangia kila kilicho chake, na yeye pia anakubaliana kuchangia na wewe kila kilicho chako, hasa laana na matatizo kama vile magonjwa na mizimu kwa sababu hivi vitu vimejengwa katika maagano ya damu.

Ndio maana wakati mnaoana na mwenzio mlipendana sana, lakini kwa sababu wewe au mwenzi wako alichepuka na kufanya maagano: ugomvi, mapigano, kutishiana, chuki na hata kutaka kuuana hakuishi kila leo! Swala sio wivu kwamba unahisi mwenzi wako anakusaliti au kuhitilafiana katika mambo tu ya kawaida, issue ni yale maagano ya damu ambayo "hudemand price"!

Mara nyingi unasikia watu wanalalamika kuhusu tabia za watoto "huyu mtoto tabia kaichukua wapi, mbona baba na mama yake au ukoo wao hawako hivyo?". Chanzo cha tabia za ajabuajabu za watoto ni matokeo ya michepuko iliyofanya maagano na watu/koo zingine zenye laana. Laana na matatizo yanayoletwa na agano la damu katika familia havihitaji mtu kuchepuka na kuzaa nje ya ndoa, bali tu kuhusiana katika mapenzi!

Mimi nilipoingia kwenye mahusiano na mke wangu nilivunja maagano yote kwa jina la Yesu. Lakini kumbuka kuwa huwezi kuvunja maagano kama vile ya michepuko kwa jina la Yesu ili "kufavor your own evil deeds"!

Maagano yanayofanywa na watu kwa njia ya mapenzi huenda vizazi hadi vizazi. Hii ni sawa kabisa kwa mjibu wa sayansi kwani "hereditary information" kutoka kizazi hadi kizazi hubebwa na viasili vilivyopo katika damu, mfano DNA.
Pasco anaweza kuendeleza hii mada kwa uchambuzi zaidi.

Mie na mke wangu tuna furaha fulltime kwa sababu mapenzi yetu yananawiri kila kukicha, na huwa hatuelewi kabisa matatizo katika ndoa za watu yanatokana na nini! "We are the happiest couple" kwa sababu "we posses several life secrets" mojawapo ni siri kuhusu agano la damu!

Tambueni ya kwamba one of the great decisions a person can make in his/her life ni kuwa na uhusiano wa kimapenzi (hata kwa dakika moja) na mtu kwa sababu anafanya naye life covenant "blood covenant"!
We teach you things that matter most!
- LifeHacker
Read More

Kila Msichana Ninae Mtongoza Ananiomba Hela...Whats This?


Mimi ni Kijana wa miaka 25 ninafanya kazi bank moja hapa Mjini ..nimefikia umri wa kutafuta mchumba wa kuoa ila hawa mabinti sijui wakoje kila ninaye mtongoza haipiti siku ananiomba hela kwa visingizio mbali mbali na mimi demu akishaniomba hela design hii hapo hapo naona sio namuona kimeo ndio wale wale ....

Kwani Mapenzi siku hizi lazima usambaze Hela kwanza ndio upendwe ama?

Naomba ushauri
Read More

Irene Uwoya Afunguka Kutokewa na ‘Mzimu’ wa Masogange


Muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya na mumewe, Dogo Janja wamefunguka sababu ya wao kuhama nyumba waliokuwa wakiishi hapo awali.

Dogo Janja amesema wamelazimika kuhama nyumba hiyo na kwenda kupanga nyumba nyingine ambayo hulipa US Dollar 800 kwa mwezi kutokana na umbali, pili mkewe, Irene alikuwa akisumbuliwa na kumbumbuka za mara kwa mara kuhusu marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.

“Nahisi kama nilikuwa namuona hivi, kwa hiyo nikashindwa, eeeh!! mara nyingi pia nahisi kama anapita hivi,” amesema Irene Uwoya.
“Of cause inaweza kuwa sababu kila akijitahidi inashindikana kwa sababu alikuwa ni mtu tumemzoea sana,” Dogo Janja ameiambia Clouds FM.
Marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam, alikuwa rafiki wa karibu sana na Irene Uwoya.
Read More

Jumatatu, 11 Juni 2018

Binti Ametupanga Wanaume Kumi na Moja na Wote Anatupa Uroda Bila Kujijua..Kipaji au Umalaya?


Ukimuona kwa macho utasema huyu ndio mwanamke kumbe ni bonge la kimeo…ilikuwa mida ya jioni natoka zangu kazini mara ikaingia massage..baby uko wapi nimekumiss…nikamjibu ndo natoka kazini now..yeye..Basi naomba upitie nyumbani japo nikuone nimekumiss sana we mwanaume.

Nikaona isiwe shida ngoja nikamuone roho yake itulie nipo njiani wazo likanijia…Nikapitia duka moja maarufu Sinza na kumnunulia zawadi ya viatu kama suprize nimejikoki mwenyewe naenda kwa babybaby…mademu bwana..!

Kufika akanipokea kwa bashasha na mabusu motomoto dady’s home..Yeye.. najua umechoka baby wangu kaa kwa kochi upumzike nataka nikutengenezee juice fresh unayo ipendaga..nikamwambia ngoja kwanza nikupe zawadi yako nikatoa vile viatu na kumpatia akafurahi sana na kuvijaribisha..vilimtosha na kumpendeza..Nikapewa busu lingine la sekunde kazaa.,

Akatoka kwenda kuandaa juice..huku simu yake na vile viatu akiwa ameviacha jirani na kochi nililokaa..Nikamuuliza simu yako inabando..akanijibu ndio..Nikaichukua nakuingia sehemu ya kubrowse internent ..akili ikanituma nifanye udukuzi kidogo nikafungua application yake ya watsupp mbona nilichoka..

Nilikuta msururu wa wanaume anaochati nao nakuwatumiana picha akiwa amevaa pichu tu nakukaa kimitego…huku wakiambiana ni jinsi gani wamemisiana kupeana utamu..kijasho kikanitoka. .nikajikaza mwenyewe na kuendelea kuperuzi kwa wote idadi ikafikia wanaume kumi na moja na kwa mtiririko wa chating yao wote waonekana wameshapewa utamu..Napenda kusema kitu kimoja hapa tangu nimeanza mahusioano nae tumefikisha mwaka sasa sikuwahi hata siku moja kuishika simu yake.,

Nilishikwa na hasira sana yani huduma zote ninazo mpatia kumbe nahudumia kahaba..nikamwita na kumuuliza aniambie hao watu ni akina nani..utetezi alionipa anasema ni marafiki zake nisimfikirie vibaya..

Nilitamani nimkate kofi moja la nguvu yani ushahidi wote ninao hapa unanijibu rejareja hivyo..nikamuuliza huo urafiki pamoja nakugongana..!we kweli kiboko sasa unataka nikupe cheo gani huu ni umalaya au kipaji...Akaanza kulia huku akiomba nimsamehe..

Kwakweli nilichanganyikiwa nakujiuliza hivi huyu binti anawezaje kutupanga wengi hivi..nilichofanya nikuchukua viatu nilivyokuja navyo nikamwambia nimejitoa kwenye hiyo cheni na kama viatu atakuleta mwingine hivi naondoka navyo..


Nipo njiani kurudi home massage za kuomba asemehewe na kuto rudia tena zinamiminika kwenye simu yangu huku akijuta na kudai mimi ndo ananipenda kiukweli nikimwacha hatopata furaha ya maisha nakuomba nimpe last chance abadirike…nikamjibu nakumwambia huwa natoa msamaha kwa makosa mengine lakini sio kwa hilo la kuchapiwa naomba tuachane kwa amani tu mama…akanipigia simu sikupokea akarudia tena na tena nikapokea..

Nikamuuliza unasemaje..akanimbia ananipenda sana na hawezi kuishi bila mimi uku akilia..nilichomjibu ni kwamba siwezi kuendelea nae.,

Kitu kingine kinacho nichanganya hapa nikwamba ametishia kujiua na yupo chini ya uangalizi wa dada yake..jamani hata kama ni msamaha nikifiria idadi yake ya wanaume nachefuka kabisa..napigiwa simu kila mara kuombwa nirudishe moyo na ndugu zake ninachowajibu ni kwamba siwezi ajaribu kumchagua mwingine atakayempenda sana..mpaka nafikia hatua ya kuwaandikia hii habari huyu binti amelazwa hospital presha imeshuka..

Hapa nafanyaje wakuu kiukweli huyu mwanamke amenitoka kabisaa..hofu yangu ni hiyo ya kulazwa kisa mimi inamaana nikigoma hata kwenda hospital..si ndio majanga yataongezeka..msaada wenu wakuu kichwa changu kimevurugwa kabisa.,
Picha Kutoka Mtandaoni
Read More

KUFURU:Gari Mpya Aina ya BMW ya Milioni 200 yatumika Kama Jeneza


Leo June 11, 2018 Mwanaume mmoja anayejulikana kama Azubuike Raia wa Nigeria amewashangaza wengi baada ya taarifa zake kusambaa kwenye mtandao wa Facebook kwamba amemzika baba yake huku akitumia gari aina BMW kama jeneza.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika zinasema kwamba gari hilo lina thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 200 za kitanzania ambalo limefukiwa chini kama jeneza ndani ya kaburi.

Aidha Mazishi hayo yalifanyika wikiendi iliyopita katika Mkoa wa Anambra nchini Nigeria ambapo ndipo yalipokuwa makazi ya baba wa Azubuike.
Read More

Alhamisi, 7 Juni 2018

Mange Kimambi Aichana Familia ya Diamond Kwa Kumdhalilisha Hamisa Mobetto Mwezi Mtukufu



From @mangekimambi_ - Unapoona familia ya kiislam hata mwezi wa Ramadhan hawana uwoga nao. Yani hata mwezi wa Ramadhan bado wanaendelea na visa, matusi, kejeli, chuki, husda, fitna, roho mbaya, dharau basi mtu inabidi uelewe unadili na watu wa aina gani.
.
.
Seriously mwezi wa Ramadhan wale bado wanachamba na kumdhalilisha mwanamke mwenzao. Yani hawana hofu ya Mungu hata mwezi huu ambao hata sisi tulioshindikana tumekituliza..Yani nashindwa hata kuwasema the way natamani niwaseme
.
.
Kutwa kuwapambanisha watoto wa wenzao huyu anajua kupika, huyu hajui, huyu mchafu, huyu msafi wao wanajua kupika? Wao wasafi? Mbona wao hawanyanyaswi au kudhalilishwa na ndugu za waume zao? Ila Mungu ni mkali sana @mama_mobetto siku hizi zilizobaki za mwezi mtukufu kazana na dua, mlilie Allah siku hizi zilizobaki. Wakabidhi kwake!! Usiwaombeee mabaya ila wakabidhi tu. Hizi dharau zote kwa wanawake wenzao sababu tu Allah kamwonyesha Neema ndugu yao?? Allah asingempa mafanikio ndugu yao je wangekuwa na dharau hizi? Hawa wanamletea nuksi ndugu yao. .
.
Pia Mungu keshaanza kujibu, Esma yuko busy na mahusiano ya kakake alafu mume wake laki moja hana mpaka anaweka passport rehani. Hizo zote ni fimbo Mungu anawachapa. Imagine kutwa mtoto wa mwenzenu yuko mdomoni alafu waume zenu laki hawana huo muda si mngeutumia kwa waume zenu ili wasiathirike? Kama nilivyosema nifimbo ya Mungu. Wao si wamemdhalilisha Hamisa sasa wao wanadhalilika mara mbili ya Hamisa.
.
.
Ila wale jamani sijui waislamu wa wapi wale. Yani hawana woga na mwezi mtukufu. Wengine hata kuandika shenzi hatuwezi ila wale wakavuuuuuuuu tena kwenye macamera, yani hawajali. Ndio sisi wote ni watenda dhambi so we cant judge each other ila muislam ambae hata mwezi mtukufu anaendelea na matendo yake ya kila siku huyo sio mzima.
Read More

Jumatatu, 4 Juni 2018

Ukimya wa Ndoa ya Kajala Wavuja


Ukimya wa Ndoa ya Kajala Wavuja
DAR Ukimuaga mtu kwamba unasafiri kwenda Zanzibar, zawadi atakayokuagiza umletee ni ubuyu. Hii inaonesha ni jinsi gani watu wanavyoupenda ubuyu!

Ubuyu wa motomoto kutoka mezani kwetu leo ni wa staa wa Bongo Muvi, Kajala Masanja ‘Kay’. Ubuyu huo unamung’unywa kwamba, hivi karibuni anataka kufunga ndoa na kigogo mmoja mwenye ‘mpunga’ mrefu, ishu hiyo imeanikwa.



Chanzo cha karibu cha staa huyo kilianza kutiririka kuwa, Kajala hivi sasa amebadili kabisa mfumo wa maisha, tofauti na alivyokuwa mwanzo.

Ilisemekana kwamba, siku hizi akishaenda kurekodi kipindi chake cha Biko, anarejea nyumbani na kujifungia muda wote.



MSIKIE MTOA UBUYU

“Kajala siku hizi kumuona ni shughuli kwa sababu muda si mrefu anaolewa na kigogo mmoja ambaye amembadilisha maisha yake.

“Ndiyo maana siku hizi huwezi kumkuta akijichanganya hata kidogo kama ilivyokuwa huko nyuma,” alisema mpashaji huyo.

Msambaza ubuyu wetu huyo alizidi kufunguka kwamba, japokuwa staa huyo nyuma alikuwa amefunga ndoa na baadaye wakapata matatizo.

“Sasa hivi huyo kigogo anayemuoa anadai ndiye mtu anayeweza kuishi naye muda mrefu. Hata hivyo, ndoa yao hiyo bado imefanywa kuwa  siri,” alisema mtoa ubuyu huyo.



KAJALA AFUNGUKA

Baada ya Ijumaa Wikienda kumwagiwa ubuyu huo, kama kawaida yake lilimtafuta Kajala ili aweke kila kitu wazi ambapo mara ya kwanza alipoulizwa kuhusu hilo alikuwa akikwepa na kumwambia mwandishi kuwa hapendelei kabisa hiyo habari kuwekwa wazi.



Mazungumzo kati ya Ijumaa Wikienda na Kajala ilikuwa kama ifuatavyo;

Ijumaa Wikienda: Vipi Kajala, naona uko bize na maandalizi ya ndoa…

Kajala: Ndoa gani au unanichuria?

Ijumaa Wikienda: Kuna ubuyu kwamba kuna kigogo mmoja anataka kukuoa na anakupa maisha (kila kitu)?



Kajala: Kwa nini mnapenda kusikiliza maneno ya waongeaji? Kama kuna mtu anataka kunioa si mtaniona ndani ya shela tu?

Ijumaa Wikienda: Kwa sababu tulijua ndoa yako ya kwanza haijavunjika, hivyo tulishangaa iweje uolewe?



Kajala: Sidhani kama kuna ndoa ilishavunjika, lakini kama kuna ndoa mtaiona tu, sioni kama kuna faida kuilezea sasa.

Ijumaa Wikienda: Lakini sasa unasemaje, hiyo ndoa ipo au haipo?

Kajala: Hilo ni jambo jema, kama lipo nitaliweka wazi siku si nyingi.
Read More

Wanaume Kwa Hili Mnatutesa Mnatuvurugia Wadada Wengi


Jamani wanaume wa kizazi hiki cha nyoka sjui mpoje, mkianza mahusiano na mtu mkapeana namba utasikia "Bby una Whatsup" Imo n.k ili uanze kudai picha za uchi na kufanya video calls. Kiukweli wadada wengi tumestukia hilo, na tunapinga vikali no video calls, no se.x pictures at all.

Kama hutaki sauti pita hivii!Kingine msitupangie matumizi ya simu zetu, hujainunua wewe sa kiherehere cha nini, kila saa umenuna"bby simu ipo busy kila saa" haikuhusu!Nunua yako nipe kisha nipangie wakuchati nao.

Picha za uchi BIG NO, USINITUMIE WALA SIKU TUMII. TUKIPANGA MIADI YA KUKUTANA NITAANDAA SEHEMU MIMI NA SIO WEWE, POTELEA MBALI KULIKO UKAFUNGE MI KAMERA ILI UNIREKODI.

KINYWAJI NI JUICE TU, POMBE SITAKII
Read More

Ijumaa, 1 Juni 2018

Sasha 'Nitaendelea Kupiga Picha za Nusu Utupu Baada ya Kupumzika Kwa Muda'


LICHA ya Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kuwafungia na kuwaita na kuwakanya wasanii ambao wamekuwa wakijianika nusu utupu, muuza nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Sasha Kassim amefunguka kuendelea kupiga picha za nusu utupu.

Akizungumza na Gazeti la Amani, Sasha alisema kuwa anajiandaa kupiga picha nyingine ambazo kama ni nguo za ndani zitaonekana nadhifu na zenye kuvutia na pia zitapungua ‘ukali’.

 “Nilipotea kwa sababu niliibiwa akaunti yangu ya Instagram, si unajua ilikuwa na picha nyingi sana ila sasa hivi najiandaa kupiga picha nyingine mpya zitakuwa zikinionyesha sehemu zangu za mwili lakini zitakuwa zenye kujistiri kidogo,” alisema Sasha
Read More

Sasha: Nitaendelea Kupiga Picha Za Utupu


Video vixen alijizolea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuanika picha za utupu siku za nyuma  Sasha  Kassim ameibuka tena  na kukiri kuwa  ataendelea kuweka picha zake za utupu mitandaoni.

Mwezi uliopita Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza alitangaza vita na wasichana wote ambao wanaanika picha zao za utupu mitandaoni na kuahidi kuwafungia kazi zao za sanaa endapo wataanika picha hizo.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu hatimaye Sasha  Kassim amefunguka kuwa ataendelea  kupiga picha za nusu uchi.

Kwenye mahojiano  na Gazeti la Amani, Sasha alisema kuwa anajiandaa kupiga picha nyingine ambazo kama ni nguo za ndani zitaonekana nadhifu na zenye kuvutia na pia zitapungua ‘ukali’.

"Nilipotea kwa sababu niliibiwa akaunti yangu ya Instagram, si unajua ilikuwa na picha nyingi sana ila sasa hivi najiandaa kupiga picha nyingine mpya zitakuwa zikinionyesha sehemu zangu za mwili lakini zitakuwa zenye kujistiri kidogo”.
Read More

Jumatano, 30 Mei 2018

Tunda na Casto Dickson Wadaiwa Kumwagana


Video vixen maarufu Bongo, Tunda Sebastian amedaiwa kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake mtangazaji wa Clouds Tv Casto Dickson.

Tetesi hizi za wawili hawa kutemana zilianza kusikika mara baada ya Tunda kufuta picha zote za wawili wao enzi za mapenzi yao.

Kipindi cha XXL cha Clouds Fm wanaripoti kuwa wawili hao wameachana na Tunda ndio kampa kibuti Casto lakini unaambiwa Casto bado anabembeleza bembeleza.

Tunda alipotafutwa kuthibitisha taarifa hiyo alikataa kuongelea Mahusiano Yake na Casto Ikiwa na pamoja kukataa kukubali kama wameachana au bado wapo wote.

Lakini pia Shilawadu wanaripoti kuwa Tunda baada ya kumwagana  na Casto alirudisha majeshi kwa mpenzi wake wa zamani Young Dee ambapo wamedai kuwa Young Dee kamuweka Tunda kama profile picture yake ya WhatsApp.

Tunda alikana taarifa hizo za kurudiana na Young Dee na kusema kamwe hatakuja kurudiana na Ex wake kwani akimaliza Mahusiano na mtu anakuwa amemaliza.
Read More

Jumatatu, 28 Mei 2018

Baada Ya Diamond, Lynn Ahamishia Majeshi Yake Kwa Chris Brown


Video vixen Irene Hillary maarufu kama Lynn aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya Rayvanny ya wimbo wa ‘Kwetu’ amefunguka kuhusu mahaba mazito kwa supastaa wa kimataifa
Read More

Jumapili, 27 Mei 2018

Kamanda Mambosasa Azungumzia 'Mabilioni ya Dr Shika'


Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema swala la Dk. shika kuingiza pesa zake Tanzania hana uhakika nalo na mtu kutumiwa hela kihalali si kosa 
Read More

Jumatatu, 21 Mei 2018

Mwanaheri: Mimi Sio Kikojozi


Muigizaji wa filamu Bongo Mwanaheri Afcely kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya tuhuma za kuwa kikojozi.

Mwanaheri amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote na watu walioanzisha hizo habari wana wivu juu ya ndoa yake.
Read More

Ijumaa, 18 Mei 2018

Mama Diamond Afunguka Kumshushia Kipigo cha Nguvu Hamisa Mobetto...Kisa Kizima Hichi Hapa


BAADA ya kuvuma kwa taarifa mitandaoni kuwa mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ amempa ‘vitasa’ mwanamitindo Hamisa Mobeto, Ijumaa limemtafuta bi mkubwa huyo na kufanya naye mahojiano maalum (exclusive) ambapo amefungukia sakata hilo kwa kirefu.
Read More

Ijumaa, 11 Mei 2018

Warembo Wazichapa Kavu Kavu Kumgombea Baba Diamond...


DARESSAL AA M: Warembo wawili ambao walifahamika kwa majina ya Ashura na Zubeda, wamedaiwa kuzichapa kavukavu chanzo kikitajwa kuwa ni kumgombea baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma.
Read More

Alhamisi, 10 Mei 2018

Hivi Ndivyo Zali Alivyozima Mbwebwe za Daimond


Hivi Ndivyo Zali Alivyozima Mbwebwe za Daimond
Dunia inakwenda spidi sana! Miezi kadhaa baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kumwagwa na mama watoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, bado mambo ni moto huku mwanamama huyo akidaiwa kuzima ngebe au mbwembwe za jamaa huyo, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.
Read More

Amber Lulu Apata Dili la Kutangaza Kondomu


Video vixen na msanii wa Bongo movie nchini Amber Lulu amekwaa dili refu la kutangaza kondomu za kiume.
Read More

Ijumaa, 27 Aprili 2018

Tunda: Huwa Sipigi Picha za Uchi


Video vixen Bongo, Tunda amedai yeye huwa hapigi picha za utupu bali watu wanavyomuona ndio mtindo wake wa maisha.

Tunda amesema picha za utupu ni pale mtu anapoenda studio na kupiga picha lakini zile anazopiga akiwa nyumbani kwake ni zinapaswa kueleweka ni picha za kawaida.

“Unajua kuna picha za utupu kwamba ile mtu unaenda studio unaamua kuwa wazi na kupiga picha, na kuna jinsi mtu anavyovaa kama ni nguo fupi yaani kawaida ya yeye kuvaa yapo si utupu kuna tofauti, mimi sipigi picha za utupu, no!,” amesema.

Tunda anametokea kwenye video za wasanii kama Young Dee, Chege na Temba na wengineo. Kwa sasa mrembo huyo katika mahusiano na mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson.
Read More

Jumatano, 18 Aprili 2018

Diva Ammwagia Mvua Ya Matusi Ya Nguoni Michael Lukindo


Msanii na mtangazaji wa kipindi cha Ala za roho cha Clouds Fm Loveness Malinzi ‘Diva The bawse’ amemtolea povu zito msanii mwenzake wa Bongo fleva Michael Lukindo ‘ML’ baada ya kudai ni wapenzi.
Read More