Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana
kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na
hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.
Jenerali
Mabeyo ametoa ushauri huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini
Bariadi Juni 07, 2018.
Mabeyo
amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na
Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye
wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya kuajiriwa .
“Vijana
tunaowachukua JKT ni kwa ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili
hata kijana akikosa nafasi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza
kurudi kijijini akafanya vitu vya maendeleo, mimi nadhani watu
wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT lazima aajiriwe, ipo
haja ya kubadili mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo
“Jeshi
linachukua vijana elfu ishirini kwa mafunzo, wanaochukuliwa na vyombo
vya ulinzi na usalama hawazidi vijana 2000 sasa hawa wengine 18,000
wanaenda wapi, kama mawazo yatakuwa ni kwenda JKT ili kuajiriwa
hatutafanikiwa lakini kama watakwenda JKT kujifunza stadi za kazi
kuwasaidia ili ziwasaidie kujiajiri na kubadili maisha yao tutafanikiwa
sana” alisisitiza
Katika
hatua nyingine Jenerali Mabeyo ametoa pongezi kwa juhudi zinazofanywa
na Mkoa wa Simiyu katika mkakati wa Kilimo cha Umwagiliaji ili kuwa na
ziada ya chakula cha kutosha.
“Suala
la umwagiliaji halikuwepo katika fikra za watu wengi, walio wengi
wanategemea mvua na isiponyesha hawalimi na maisha yanakuwa duni
wanaanza kuilalamikia Serikali, lakini sisi hapa tunayo maji ya Ziwa
Victoria, Mkuu wa Mkoa nawapongeza sana kwa juhudi zinazofanywa katika
kilimo cha Umwagiliaji, zitasaidia kuwatoa wananchi kwenye ufukara”
amesema Mabeyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema mkoa huo
umeweka malengo ya kujitosheleza kwa chakula na kupitia mkakati wa kuwa
na mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Mwamanyili wilayani
Busega, ambapo amebainisha kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo imeahidi
kutoa shilingi bilioni 12kwa ajili ya mradi huo.
“
Lengo letu kama mkoa ni kuifanya wilaya ya Busega kuwa eneo ambalo
linafanya vizuri katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa lina maji ya
uhakika ya Ziwa Victoria, Benki ya Kilimo wameahidi kutupa shilingi
bilioni 12 kwa ajili ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Mwamanyil”
alisema Mtaka.
Akizungumzia
suala la elimu Mtaka amesema mkoa huo umejipanga kiushindani ambapo
madarasa ya mitihani. yatakuwa na makambi ya kitaaluma ambazo
zitawakutanisha wanafunzi kwa ajili ya kupitia maeneo yaliyo magumu ili
waweze kujiandaa vema na mitihani ya Kitaifa.
MWISHO
0 comments:
Chapisha Maoni