Mfanyakazi
wa ndani aliyemuua mwajiri wake pamoja na mtoto wake mwenye miezi
mitatu huko Muhoroni, Kisumu nchini Kenya na kutokomea kusikojulikana
amekamatwa Uganda na jeshi la polisi la nchi hiyo.
Jacky
Auma alikamatwa katika eneo la Namayisi nchini Uganda baada ya jeshi la
Polisi nchini Kenya kuwapa taarifa juu ya mtuthumiwa huyo kukimbilia
katika mipaka ya nchi hio.
Jacky
anatuhumiwa kutenda tukio hilo wiki iliyopita kwa kumpiga mtoto wa
mwajiri wake mpaka kufa kisha akamchoma mwajiri wake na kisu mara kadhaa
kabla ya kumchoma na kitu kinachodhaniwa kuwa ni pasi ya umeme au
tindikali na kumfanya apoteze uhai wake.
Aidha
Afisa Polisi wa kituo cha Busia amethibitisha kukamatwa kwa Jacky na
amesema kuwa wako wanaandaa utaratibu ili mtuhumiwa huyo arudishwe
nchini Kenya akafunguliwe mashitaka.
0 comments:
Chapisha Maoni