Mabingwa wa ligi
kuu ya Tanzania Simba wametolewa jasho naa Kariobangi Sharks ya Kenya
kabla ya kuibuka mshindi kwa mabao 3-2 ya penalti.
Hii ni baada ya
sare tasa katika mashindano ya kandanda ya SportPesa Super Cup kwenye
uwanja wa Afraha mjini Nakuru eneo la Bonde la Ufa Jumatatu. Nusra Papa hao wa Kariobangi wameze Simba lakini Jonas Mkude akawapatia mabingwa mara 19 wa ligi kuu ya Tanzania ushindi kwa kufunga bao muhimu lililowawezesha Wekundu wa Msimbazi kufuzu kwa nusu-fainali.
Sasa Simba watakutana na Kakamega Homeboyz ya Kenya Alhamisi wiki hii..
Matokeo ya mechi za sasa
- Kakamega Homeboyz 3-1 Yanga
- Gor Mahia 3-0 JKU
- Simba 3-2 Kariobangi Sharks
0 comments:
Chapisha Maoni