Mbunge
wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye pia ni msanii nguli na
mkongwe kwenye game ya hip hop ya bongo, anatarajia kuachia kazi yake
mpya hivi karibuni aliyoipa jina la namba yake ya jela, 219.
Sugu
anaachia wimbo huo ikiwa zimepita siku 25 tangu alipotoka gerezani kwa
msamaha wa Rais John Magufuli, Mei 10, 2018, na kusema kwamba wimbo huo
utabeba mambo mbali mbali aliyokutana nayo akiwa jela kama mfungwa.
“Maandalizi
na kila kitu kipo poa na soon nitautoa wimbo wangu nilioupa jina la
219, nimeimba mimi mwenyewe na nimezungumzia hali ya nchi, experience
yangu niliyoipata gerezani na mambo mengine, ni ngoma nzuri kabisa”,
amesema Sugu.
Sugu amesema ameamua kuita jina hilo la namba yake ya ufungwa kwa sababu ni namba inayojulikana nchi nzima.
0 comments:
Chapisha Maoni