Watafiti wa Kizungu wanakesha kufanya tafiti chungu mzima na zingine majibu yake zinaweza kukuacha mdomo wazi.
Kwa
mfano huu – jamaa eti wamebaini kuwa kushiriki tendo la ndoa mara
nyingi kunaongeza imani ya kiroho na hata imani kwa Mungu! Makubwa..
Kwa
mujibu wa utafiti, tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo iitwayo
oxytocin ambayo haiishi tu kutengeneza ukaribu wa kijamii bali pia imani
ya Mungu – hususan kwa wanaume.
Watafiti
katika chuo kikuu cha Duke cha North Carolina, wanasema kuwa tendo hilo
huhamasisha imani – ama kuongeza imani katika Mungu na dini.
Utafiti
huo umeliochapishwa mwishoni mwa wiki unaangalia homoni ya oxytocin
ambayo huamshwa zaidi wakati wa kufanya mapenzi, wakati wa kuzaa na
wakati wa kunyonyesha.