Kamanda
wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema swala
la Dk. shika kuingiza pesa zake Tanzania hana uhakika nalo na mtu
kutumiwa hela kihalali si kosa
Amesema kuwa kama taarifa hizo ni za uongo anaweza kupuuzwa ila endapo kauli yake italeta madhara basi hatua zitachukuliwa.
Mambosasa
amezungumza hayo leo pindi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari
akitoa ripoti za jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa mbambali kwa
kufanya makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha za moto.
”Mtu
kutumiwa hela kama ni halali haziingii kwenye pesa ambazo
zinatakatishwa au hela ambazo zinapatikana kwa njia isiyo halali si kosa
lakini kama ni muongo tu anajisema basi kuna mawili anaweza kupuuzwa
lakini kama kauli zake zitamwaathiri yeyote anaweza kuja kulalamika na
jeshi la polisi likachukua hatua” amesema Mambosasa.
Mambosasa
amezungumza hayo pindi alipokuwa anajibu swali la mmoja wa waandishi wa
habari baada ya kuhoji juu ya uhalali wa pesa za Dk. Luis Shika ambaye
hivi karibuni taarifa zimeeleza tayari ameingiza mabilioni yake ya fedha
nchini Tanzania.
Siku
chache zilizopita Dkt. Louis Shika alivieleza baadhi ya vyombo vya
habari nchini juu ya ujio wa fedha zake na baadhi ya vipande vya dhahabu
zilizokuwa nje ya nchi kuwa tayari zimewasili nchini kupitia Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA) na
kupelekwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ajili ya kuhakikiwa.
Taarifa
hizo zilizua mjadala mkubwa mtandaoni ambapo watu walionesha
kutokuamini kwa ujio huo wa pesa za Dk. Shika wakidhani ni stori zisizo
na ukweli ndani yake.
Hata hivyo Shika alithibitisha ujio wa mali hizo na kuonyesha baadhi ya nyaraka zinazothibitisha umiliki wa mali hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni