test
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo WASANII. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo WASANII. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 22 Juni 2019

VEDIO MPYA: Simama na Mungu By Shalom band (Official video)


Read More

Jumapili, 10 Februari 2019

Jumanne, 12 Juni 2018

Zari Akana Kurudiana Kimapenzi na Diamond


Kufuatia video ya wimbo wa msanii wa bongo fleva nchini Diamond kutoka akiwa amemshirikisha Rayvany na kibao chao cha Iyena kumekuwa na mvumo wa maneno mengi yakidai kuwa kuonekana kwa Zarinah Hassan katika video hiyo kumedhihirisha wazi kuwa wawili hao wamerudiana.

Zari kupitia ukurasa wake wa instagram ameamua kuzima uvumi huo kwa kuweka wazi kuwa uhusiano uliopo kati yake na baba watoto wake, Diamond Platinumz ni kama wazazi tu na si vinginevyo.

Amesema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya watoto wao hivyo mashabiki wao waelewa hivyo na kwamba wanawapenda sana.

”Just to clear the air, we are not back together but have agreed on co-parenting as per my break up post that will remain great parents to our lovely kids. Just a lil note to all our fans. We love you too.

Utakumbuka hivi karibuni meneja wa Diamond, Babu Tale alienda Afrika Kusinia ambapo anaishi Zari ili kusuluhisha tofauti za wawili hao. Hakuna yeyote kati yao aliyetoa jibu la uhakikika iwapo mahusiano hayo yamerudi zaidi ya hiki alichoeleza Zari .

Katika mahusiano yao Zari na Diamond walijaliwa kupata watoto wawili ambao ni Tiffah na Nillan. Zari ndiye aliyetangaza kuvunja mahusiano na Diamond kwa kile alichodai muimbaji huyo alikuwa akimvunjia utu wake kwenye mitandao.
Read More

Diamond Athibitisha Kumnunulia Mjengo Hamisa


Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amethibitisha tetesi zilizokuwa zinasambaa mtandaoni kuwa amemnunulia mjengo mma watoto wake Hamisa.

Baada ya Diamond kuachana na Zari na Kurudisha majeshi kwa Hamisa imekuwa ikisemekana kuwa Hamisa amehama alipokuwa anaishi na kuhamia kwenye mjengo mpya kabisa na mtoto wake Dylan na Fantasy.


Taarifa zilisambaa kuwa mjengo wenyewe ni ghorofa  ambalo ni bonge wa mjumba ambao upo maeneo ya Mbezi Beach, Bahari Beach. Diamond amethibitisha taarifa baada ya kuandika Instagram na Hamisa kujibu kwa kumshukuru kwa nyumba hiyo:

Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kununua Nyumba kwa ajili ya wanafamilia wake kama utakumbuka ameshawahi kumnunulia nyumba mama yake mzazi Lakini pia ameshamnunulia nyumba mzazi mwenzake Zari nchini South Africa.
Read More

Jumatatu, 11 Juni 2018

Zari: “Hamisa Hata Akitaka Kuzaa Watoto Kumi na Diamond Azae Tu”


Mfanyabiashara maarufu na mama watoto wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan amemwaga povu na kusema Hamisa hata akitaka kumzalia watoto kumi Diamond yeye kwake ruksa.

Zari ametoa kauli hiyo jana baada ya kuweka posti yake aliyokuwa anasherehekea kufikisha followers milioni 4 Kwenye mtandao wa Instagram ambapo shabiki alimtahadharisha kuwa kuna tetesi Hamisa ana ujauzito mwingine.

"Zari kuwa makini kuna tetesi huku mtaani kwetu kuwa Hamisa kashanasa mimba nyingine ila lisemwalo lipo kama halipo laja”.Aliandika shabiki huyo

Baada ya kupewa maneno hayo Zari alimjibu hata wangezaa watoto kumi yeye hana habari kwani hayumo.

Zari alijibu kwa kuandika:" Azae hata kumi mimi simo!”.

Huu ni muendelezo tu wa drama iliyoanza mwaka jana baada ya Hamisa kubeba mimba ya  Diamond

Kumekuwa na tetesi  kuwa Diamond amerudisha majeshi kwa mama watoto wake Zari baada ya kuachana na  kutoonana kwa muda mrefu
Read More

Alhamisi, 7 Juni 2018

TANZIA:Msanii Samu wa Ukweli afariki Dunia


Mwanamuziki wa Bongo Fleva "SAM WA UKWELI" amefariki dunia usiku wa kuamkia leo June 7 katika Hospitali ya Palestina "Sinza" jijini Dar es salam


mwili wa marehemu umehamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.


SAM WA UKWELI ni msanii aliyewahi kutamba Sana na ngoma kama Sina Raha na nyingine kibao .


Inna lillahi wa inna ilaihi rajioon
Read More

Zari Akubali Kurudiana Diamond


Baada ya masaa takribani 13,tangu hit maker wa African Beuty na King of Pop in Afrika ambaye bado anasumbua na ngoma aliyoshirikishwa na harmonize "Kwangwaru,Diamond Platnumz maarufu kama Chibu Dee kuachia kichupa cha karne "Iyena" hatimaye Star wa Manzese True Boy "Nay wa mitego ameibuka na kumwagia sifa kijana huyo ambaye leo amenunua :D:Dpage zote za instagram na youtube kwa kazi nzuri ya wimbo huo uliopo kwenye album ya A boy from Tandale.

Katika post yake huko IG Nay amesifia kazi nzuri na kumlaumu Diamond kwa kupuyanga na "Mapugi machafua nyota" .

Aidha,Nay amesema anafanya mpango aongee na mama Tee ili yaishe jambo hilo limemfurahisha Zari ambapo amelike na Kukomenti post hiyo kwa kuweka emoji ya Kusalimu amri...

Je hii ni ishara kwamba Mama Nillan yuko tayari kurudi Madale?
Read More

Jumatatu, 4 Juni 2018

Angel Mary Awatamani Vannesa na Alikiba.


Msanii wa muziki Bongo, Angel Mary amefunguka kuhusu mipango yake ya kimuziki kwa miaka ya mbeleni.

Muimbaji huyo amesema moja ya ndoto zake ni kuweza kuiwakilisha Bongo Flava na Tanzania kiujumla kimataifa kama wanavyofanya Alikiba na Vanessa Mdee.

“Angalau miaka mitatu/mitano mbeleni muziki wangu uwafikie sio Watanzania tu, sio East Afrika tu, yaani dunia nzima. Nipate kuwa mmoja wapo ya wasanii ambao tunaona kama Vanessa Mdee, Alikiba ambao wanapeperusha bendera ya Tanzania vizuri sana,” Angel ameiambia Clouds TV.

Ameendelea kwa kusema kuwa kufanya hivyo inakuwa kama chanzo cha kujivunia kuwa Mtanzania kwa kuona kwamba tunafanya kitu kizuri. Kwa sasa Angel Mary ambaye ni zao la BSS anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la Magongo.
Read More

Diamond Platnumz: Mwanamke Sura Kwanza.... Tabia Baadae


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa yeye kigezo kikubwa anachotumia kumpata mwanamke mwema wa kuoa ni kuangalia sura na sio tabia kama wengi wanavyosema.

Diamond akitetea msimamo wake kwenye kipindi cha Kaa Hapa kinachorushwa TBC 1, amesema kuwa mwanamke huwezi kumbadilisha sura kwa namna yoyote ile lakini tabia ni rahisi kumbadilisha.

Akielezea kuhusu kigezo hicho, Diamond amesema kama angetoa asilimia kwa vigezo vya sura na tabia basi asilimia 70 angetoa kwa upande wa sura na asilimia 30 zilizobaki ndio angeangalia tabia.

“Kiukweli tabia tunapenda lakini wakati mwingine sura nazo zina uzito wake, Kiukweli tabia mnaweza kuelekezana ila sura kuelekezwa mtaelekezana vipi?. Tabia tunajifunza kama alijifunza kuchukia atajifunza kupenda, sura atajifunza vipi?, Kwa mwanamke mimi naangalia sura kwanza , tabia tutaelekezana.“amesema Diamond Platnumz.

Hata hivyo, kupitia kipindi hicho Diamond Platnumz amefunguka kuhusu zile picha za faragha zilizovuja akiwa na Hamissa Mobetto kwa kusema kuwa walikuwa location wakirekodi kipindi cha TV.

Read More

Shamsa Ford Awapa Makavu Wakina Aunt Ezekiel


Shamsa Ford Awapa Makavu Wakina Aunt Ezekiel
MWANAMAMA wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amewavaa na kuwaponda wakongwe wenzake wa tasnia hiyo kwa maelezo kwamba hawana jipya hivyo kutaka sura mpya kujitokeza kwenye fani hiyo.



Shamsa alifunguka ishu hiyo wiki iliyopita alipokuwa akifanya usahili wa wasanii chipukizi watakaouza nyago kwenye sinema mpya iitwayo Saa Imetimia inayoratibiwa na mdau wa Bongo Muvi na mwanaharakati, Lilian Wassira.



Shamsa aliwataja mastaa wakubwa kama Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na wengineo kuwa wanashindwa kuonesha jipya kwenye tasnia hiyo na kuwafanya mashabiki kuhamia kwenye sinema za nje.
Read More

Chris Brown Aanza Kujirudisha kwa Rihanna


Chris Brown Aanza Kujirudisha kwa Rihanna
Ukisema cha nini wenzako wanasema watakipata lini. Chris Brown ameanza kuwasha taa ya kijani kumfukuzia upya Rihanna.

Chris amemfollow Rihanna kwenye Instagram ikiwa ni muda mfupi baada ya taarifa za mrembo huyo kuachana na mpenzi wake, Hassan Jameel.

Hatua hiyo ya Chris imeonekana kama bado anamfukuzia mrembo huyo ambaye aliwahi kummiliki mwaka 2007 na walimwagana 2009.

Rihanna na Hassan ambaye ni tajiri wa Saudi Arabia wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tangu Juni mwkaa jana, ila imeripotiwa kuwa kwa sasa wameachana na Rihanna ndiye aliyevunja mahusiano hayo.
Read More

Harmonize: Siwezi Kumchagulia Diamond Mwanamke wa Kuoa, Aoe Yeyote, Kwani Utamu Ntapata Mimi ?


Harmonize: Siwezi Kumchagulia Diamond Mwanamke wa Kuoa, Aoe Yeyote, Kwani Utamu Ntapata Mimi ?
Diamond Platnumz bado amezid kukamata headline mitandaoni kuhusu maisha yake  ya kimahusiano, safari hii Harmonize naye katia neno katika hayo yanayoendelea.

Harmonize amesema hawezi kumshauri Diamond Platnumz awe na nani kwa sasa kati ya Zari, Hamisa au Wema ila ataonesha ushirikiano kwa yeyote akayechaguliwa na Diamond.

“Mimi yeyote; akiniambia leo tunarudi South Africa mimi nipo pale Pretoria, akiambia kwa wakati huu tuhamie Ununio, nipo pale kwa Madam, akiambia official tunachukua Hamisa tunaweka ndani nipo, sasa jamani kwani utamu napata mimi,” Harmonize ameiambia Wasafi TV.

Awali Harmonize alisema kuwa licha ya kufanya kazi na Diamond kwa ukaribu na kusaidiana  katika mambo mbali mbali ni vigumu kwa yeye kumshauri kuhusu mahusiano yake ila watu wa karibu kutoka kwenye familia yake kama Romy Jons na Esma Platnumz wanaweza kufanya hivyo.
Read More

Muna Afunguka Ndoa na Mwimbaji wa Injili Joel Mwanga


MWIGIZAJI wa Bongo Movu ambaye kwa sasa amezipa kisogo baada ya kuokoka, Rose Alphonce ‘Muna’ amefungukia madai ya kuwa anatoka kimapenzi na staa wa nyimbo za Injili Bongo, Joel Mwanga na kwamba anataka kufunga naye ndoa.

 Akizungumza na Over Ze Weekend, Muna alisema kuwa, ishu hiyo imemchafua yeye na Joel kanisani wanakosali, kwani Joel ni mmoja wa watu waliomfanya hadi sasa kusimama kwenye wokovu na si vingine kama watu wanavyosema.

 “Jamani huyo Joel wanayesema kuwa mimi ndiye mtu wangu wanakosea. Joel ndiye aliyenifundisha wokovu. Kwa kweli maneno hayo ya uwongo yananiuma sana, yanamchafua kaka wa watu bila sababu na kunifanya nionekane wa ajabu bila ukweli wowote,” alisema Muna.
Read More

Jumamosi, 2 Juni 2018

Tazama Video Mpya ya Wimbo wa Rosa Ree Feat Emtee Kutoka South Africa



Tazama Video Mpya ya Wimbo wa Rosa Ree Feat Emtee Kutoka South Africa

Bonyeza hapo chini kutazama Video hiyo:

Read More

Ijumaa, 1 Juni 2018

VIDEO: Nitaolewa Mungu Akinipa Mume Nina Hisia na Mimi, Diamond Atasubiri - Queen Darleen


Msanii kutoka lebo ya WCB ambae pia ni Dada wa Diamond Platnumz, Queen Darleen ambae ametamba na ngoma ya Touch ambayo imetengezwa na studio ya Wasafi, amesema kuwa yeye pia ana hisia na upendo na anapenda hivyo kuhusiana na yeye kuwa na ndoa Ataolewa hadi mungu atakapompatia, na Diamond atasubiri sana hadi yeye aolewe.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI:
Read More

Sasha 'Nitaendelea Kupiga Picha za Nusu Utupu Baada ya Kupumzika Kwa Muda'


LICHA ya Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kuwafungia na kuwaita na kuwakanya wasanii ambao wamekuwa wakijianika nusu utupu, muuza nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Sasha Kassim amefunguka kuendelea kupiga picha za nusu utupu.

Akizungumza na Gazeti la Amani, Sasha alisema kuwa anajiandaa kupiga picha nyingine ambazo kama ni nguo za ndani zitaonekana nadhifu na zenye kuvutia na pia zitapungua ‘ukali’.

 “Nilipotea kwa sababu niliibiwa akaunti yangu ya Instagram, si unajua ilikuwa na picha nyingi sana ila sasa hivi najiandaa kupiga picha nyingine mpya zitakuwa zikinionyesha sehemu zangu za mwili lakini zitakuwa zenye kujistiri kidogo,” alisema Sasha
Read More

Bado Lulu ‘anamchanganya’ Bahati kutoka Kenya


Kitendo cha Elizabeth Michael ‘Lulu’ kumuweka msanii Bahati kutokea Kenya hotelini kinyume na makubaliano yao, bado hakimtoki kichwani muimbaji huo wa gospel.

Kwa mujibu wa Bahari mwaka 2016 alikuja Tanzania kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake ‘Maria’ na alipanga kumtumia Lulu kama video vixen, hata hivyo mrembo huyo hakutokea katika kikao walichopanga kingefanyika hotelini.

Kwa sasa Bahati amerudi tena Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi na msanii wa WCB, Mbosso, hata hivyo bado anakumbuka alichofanyiwa na Lulu.

“Ilikuwa meeting ya video vixen, kama alinifanyia hivyo je anayempenda inakuwaje?, na mimi nilikuwa nimeweka shilingi kidogo, naongea kwa uchungu,” amesema Bahati hapo jana mara alipowasili Bongo.

Soma Pia; Bahati asimulia kilichomtokea kwa Lulu

Hata hivyo baada ya kutompata Lulu, Bahati alikuja kufanya video hiyo na Jokate Mwegelo.

Kabla ya tukio hilo kutokea, hapo awali muimbaji huyo aliwahi kueleza hisia zake kwa Lulu kupitia vyombo vya habari kwa kueleza kuwa iwapo atampata mrembo huyo atakuwa ametulia kabisa.
Read More

Hapa kuna Mbuzi na Kuku Lazima Tuheshimiane- Steve Nyerere


Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, ameingilia kati ugomvi baina ya Duma na Gabo Zigamba huku akimtaka Duma kuachana na masuala hayo kwa kuwa anaetaka kushindana naye yupo juu yake zaidi kwa kila kitu.


Steve ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV huku akionekana kukerwa na kitendo hicho ambacho kimedumu kwa muda mrefu kwa wawili hao na kupelekea Steve kuwafananisha na wanyama aina ya mbuzi na kuku kutokana na tabia zao.

"Hapa katikati kuna mbuzi na kuku, lazima tuheshimiane kutokana na urefu na hata jinsi mbuzi anapochinjwa kilo zake huwa kubwa na kilo za kuku ni ndogo. Kwa hiyo lazima waheshimiane hata kwa kilo, ukuaji. Wasifikilie kwamba ugomvi wanapokuwa wanagombana ulaya basi nasi Afrika tufanye ili tuuze sokoni maana wengine wanasema kugombana ni kiki, na kataa hilo muda mwingine ni kudhalilishana tu", amesema Steve.

Pamoja na hayo, Steve Nyerere ameendelea kwa kusema "heshima sio lazima uwe umetokanayo nyumbani kwenu hata unapokuwa heshima unakuwa nayo ili upate kumuheshimu kila mmoja upate connection na maisha ya kesho na kesho kutwa".
Read More