Dkt.
Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la
kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, amefunguka na kutangaza
nia ya kujihusisha na masuala ya muziki nchini Tanzania hasa upande wa
kuwasimamia wasanii wachanga na wakubwa.
Dkt.
Shika ametoa kauli hiyo leo Juni 08, 2018 wakati alipokuwa anazungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema siku si nyingi
atatangaza jina rasmi ya label yake ambayo itakuwa inajuhusisha na
kusimamia kazi za wasanii wa BongoFleva huku akidai lengo lake kubwa ni
kutaka kutimiza ndoto za kila mmoja kupitia sanaa.
"Sasa
tutaelewana tu na kabla hatujaanza na masuala ya viwanda 30 nilivyo
vitaja na 'different services', kwa sasa ninaanza na 'music industry' na
tunaanzia kwa msanii mmoja ambaye anaitwa Godson anayetokea Songea na
hili nina uhakika watanzania watafurahi na kufuta 'stress' mbalimbali
zilizokuwa zinawasumbua", amesema Dkt. Shika.
Pamoja
na hayo, Dkt. Shika ameendelea kwa kusema "nipo tayari kuwasimamia
wasanii wengine watakaopenda lakini ninaanza na huyu mmoja na nina
uhakika atawafunika wasanii wengi, kwa hiyo jaribuni kumfuatilia".
Kwa
upande mwingine, Dkt. Louis Shika amesema ukimya wake wa kipindi kirefu
umetokana na yeye kuhangaikia kuingiza fedha nchini kutokea nje ili
aweze kutimiza azma yake aliyokuwa ameitangaza hapo awali.
0 comments:
Chapisha Maoni