Skip to content
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameongoza
waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa Mapacha walioungana Maria na
Consolata mkoani Iringa amabapo alizungumza na waandishi wa habari na
kusema mapacha hao Maria na Consolata ni mashujaa wa Taifa na kwamba
wameliacha taifa katika simanzi nzito.
"Mara ya mwisho niliwaona
pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa mahututi, inaniumiza mno lakini
mapenzi ya Mungu yatimizwe," amesema.
Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu waliokuwa wakipigania elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo.
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx
0 comments:
Chapisha Maoni