Steve ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV huku akionekana kukerwa na kitendo hicho ambacho kimedumu kwa muda mrefu kwa wawili hao na kupelekea Steve kuwafananisha na wanyama aina ya mbuzi na kuku kutokana na tabia zao.
"Hapa katikati kuna mbuzi na kuku, lazima tuheshimiane kutokana na urefu na hata jinsi mbuzi anapochinjwa kilo zake huwa kubwa na kilo za kuku ni ndogo. Kwa hiyo lazima waheshimiane hata kwa kilo, ukuaji. Wasifikilie kwamba ugomvi wanapokuwa wanagombana ulaya basi nasi Afrika tufanye ili tuuze sokoni maana wengine wanasema kugombana ni kiki, na kataa hilo muda mwingine ni kudhalilishana tu", amesema Steve.
Pamoja na hayo, Steve Nyerere ameendelea kwa kusema "heshima sio lazima uwe umetokanayo nyumbani kwenu hata unapokuwa heshima unakuwa nayo ili upate kumuheshimu kila mmoja upate connection na maisha ya kesho na kesho kutwa".
0 comments:
Chapisha Maoni