Msanii
wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa yeye kigezo
kikubwa anachotumia kumpata mwanamke mwema wa kuoa ni kuangalia sura na
sio tabia kama wengi wanavyosema.
Diamond
akitetea msimamo wake kwenye kipindi cha Kaa Hapa kinachorushwa TBC 1,
amesema kuwa mwanamke huwezi kumbadilisha sura kwa namna yoyote ile
lakini tabia ni rahisi kumbadilisha.
Akielezea
kuhusu kigezo hicho, Diamond amesema kama angetoa asilimia kwa vigezo
vya sura na tabia basi asilimia 70 angetoa kwa upande wa sura na
asilimia 30 zilizobaki ndio angeangalia tabia.
“Kiukweli
tabia tunapenda lakini wakati mwingine sura nazo zina uzito wake,
Kiukweli tabia mnaweza kuelekezana ila sura kuelekezwa mtaelekezana
vipi?. Tabia tunajifunza kama alijifunza kuchukia atajifunza kupenda,
sura atajifunza vipi?, Kwa mwanamke mimi naangalia sura kwanza , tabia
tutaelekezana.“amesema Diamond Platnumz.
Hata
hivyo, kupitia kipindi hicho Diamond Platnumz amefunguka kuhusu zile
picha za faragha zilizovuja akiwa na Hamissa Mobetto kwa kusema kuwa
walikuwa location wakirekodi kipindi cha TV.
0 comments:
Chapisha Maoni