Staa
wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amethibitisha tetesi
zilizokuwa zinasambaa mtandaoni kuwa amemnunulia mjengo mma watoto wake
Hamisa.
Baada
ya Diamond kuachana na Zari na Kurudisha majeshi kwa Hamisa imekuwa
ikisemekana kuwa Hamisa amehama alipokuwa anaishi na kuhamia kwenye
mjengo mpya kabisa na mtoto wake Dylan na Fantasy.
Taarifa
zilisambaa kuwa mjengo wenyewe ni ghorofa ambalo ni bonge wa mjumba
ambao upo maeneo ya Mbezi Beach, Bahari Beach. Diamond amethibitisha
taarifa baada ya kuandika Instagram na Hamisa kujibu kwa kumshukuru kwa
nyumba hiyo:
Hii
sio mara ya kwanza kwa Diamond kununua Nyumba kwa ajili ya wanafamilia
wake kama utakumbuka ameshawahi kumnunulia nyumba mama yake mzazi Lakini
pia ameshamnunulia nyumba mzazi mwenzake Zari nchini South Africa.
0 comments:
Chapisha Maoni