test

Jumanne, 12 Juni 2018

Zari Akana Kurudiana Kimapenzi na Diamond


Kufuatia video ya wimbo wa msanii wa bongo fleva nchini Diamond kutoka akiwa amemshirikisha Rayvany na kibao chao cha Iyena kumekuwa na mvumo wa maneno mengi yakidai kuwa kuonekana kwa Zarinah Hassan katika video hiyo kumedhihirisha wazi kuwa wawili hao wamerudiana.

Zari kupitia ukurasa wake wa instagram ameamua kuzima uvumi huo kwa kuweka wazi kuwa uhusiano uliopo kati yake na baba watoto wake, Diamond Platinumz ni kama wazazi tu na si vinginevyo.

Amesema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya watoto wao hivyo mashabiki wao waelewa hivyo na kwamba wanawapenda sana.

”Just to clear the air, we are not back together but have agreed on co-parenting as per my break up post that will remain great parents to our lovely kids. Just a lil note to all our fans. We love you too.

Utakumbuka hivi karibuni meneja wa Diamond, Babu Tale alienda Afrika Kusinia ambapo anaishi Zari ili kusuluhisha tofauti za wawili hao. Hakuna yeyote kati yao aliyetoa jibu la uhakikika iwapo mahusiano hayo yamerudi zaidi ya hiki alichoeleza Zari .

Katika mahusiano yao Zari na Diamond walijaliwa kupata watoto wawili ambao ni Tiffah na Nillan. Zari ndiye aliyetangaza kuvunja mahusiano na Diamond kwa kile alichodai muimbaji huyo alikuwa akimvunjia utu wake kwenye mitandao.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni