Mahakama
ya Hakimu Mkazi ya Bukombe mkoani Geita imemhukumu Mwalimu wa Shule ya
Msingi Umoja, Daniel Nyingati kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini
ya Sh milioni 1.6 baada ya kupatikana na makosa ya kuomba na kupokea
rushwa.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukombe, Gabriel Kurwijila.
Alisema
mshitakiwa Nyingati amekutwa na hatia ya kuomba rushwa ya Sh 130,000
kutoka kwa Marco Elias aweze kumdahili mtoto wake aliyekuwa amehitimu
masomo ya shule ya msingi kinyume na sheria.
Hakimu
Kurwijila alisema ushahidi ulitolewa mahakamani pande zote mbele ya
waendesha mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa
Tanzania (Takukuru), Kelvin Murusuri na Husna Kiboko umejitosheleza na
kumtia hatiani mwalimu Nyingati.
Alisema
mahakama inamhukumu mwalimu Nyingati kwenda jela miaka mitatu au kulipa
faini ya Sh milioni 1.6 kwa kuwa alitenda kosa la kuomba na kupokea
rushwa.