Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa ufafanuzi kuhusu uwekaji
wa alama za X na kuvunja majengo yanayojengwa katika miji bila kibali
na katika viwanja vya watu wengine walio na hati miliki za ardhi kwa
dhuluma.
Taarifa
ya wizara iliyotolewa leo Jumatatu Oktoba 23,2017 imesema kwa wale
waliojenga kwenye viwanja vyenye hati za watu wengine kwa nguvu na
kuwadhulumu wenye hati miliki haki yao ya kisheria, hatua zitachukuliwa
ili kuwarudishia haki wanaostahili.
“Hatutabomoa
nyumba ya mtu bali tutaendelea na urasimishaji wa makazi kwa maeneo
yaliyojengwa holela ili yawe makazi rasmi na wananchi wapelekewe huduma
muhimu kama vile barabara, umeme na maji,” imesema taarifa hiyo.
Wizara
imesema, “Muhimu wapewe hati miliki ili ziwasaidie kiuchumi na waweze
kulipa kodi ya ardhi... lakini tutazuia ujenzi mpya holela katika miji
yetu kwa mujibu wa sheria.”
Taarifa
imesema viongozi wote wa wilaya na mitaa wahamasishe wananchi kushiriki
kikamilifu katika urasimishaji wa makazi yao kwa faida yao na Taifa kwa
jumla.
0 comments:
Chapisha Maoni