test

Jumatatu, 4 Juni 2018

Muna Afunguka Ndoa na Mwimbaji wa Injili Joel Mwanga


MWIGIZAJI wa Bongo Movu ambaye kwa sasa amezipa kisogo baada ya kuokoka, Rose Alphonce ‘Muna’ amefungukia madai ya kuwa anatoka kimapenzi na staa wa nyimbo za Injili Bongo, Joel Mwanga na kwamba anataka kufunga naye ndoa.

 Akizungumza na Over Ze Weekend, Muna alisema kuwa, ishu hiyo imemchafua yeye na Joel kanisani wanakosali, kwani Joel ni mmoja wa watu waliomfanya hadi sasa kusimama kwenye wokovu na si vingine kama watu wanavyosema.

 “Jamani huyo Joel wanayesema kuwa mimi ndiye mtu wangu wanakosea. Joel ndiye aliyenifundisha wokovu. Kwa kweli maneno hayo ya uwongo yananiuma sana, yanamchafua kaka wa watu bila sababu na kunifanya nionekane wa ajabu bila ukweli wowote,” alisema Muna.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni