Msanii wa muziki Bongo, Angel Mary amefunguka kuhusu mipango yake ya kimuziki kwa miaka ya mbeleni.
Muimbaji
huyo amesema moja ya ndoto zake ni kuweza kuiwakilisha Bongo Flava na
Tanzania kiujumla kimataifa kama wanavyofanya Alikiba na Vanessa Mdee.
“Angalau
miaka mitatu/mitano mbeleni muziki wangu uwafikie sio Watanzania tu,
sio East Afrika tu, yaani dunia nzima. Nipate kuwa mmoja wapo ya wasanii
ambao tunaona kama Vanessa Mdee, Alikiba ambao wanapeperusha bendera ya
Tanzania vizuri sana,” Angel ameiambia Clouds TV.
Ameendelea
kwa kusema kuwa kufanya hivyo inakuwa kama chanzo cha kujivunia kuwa
Mtanzania kwa kuona kwamba tunafanya kitu kizuri. Kwa sasa Angel Mary
ambaye ni zao la BSS anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la Magongo.
0 comments:
Chapisha Maoni