Jungukuu leo
MAHAKAMA
ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara imemuhukumu kifungo
cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 24, mwanafunzi wa kidato cha tatu
katika shule ya sekondari Bukanga kwa unyang’anyi wa kutumia silaha.
Joseph
Marigeri (21) ambaye alidaiwa kufanya unyang’anyi katika Kata ya
Makoko Manispaa ya Musoma,alihukumiwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama
hiyo, Baraka Maganga.
Awali
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wakili Ally Mbogoro alieleza kuwa
mwanafunzi huyo alitenda kosa hilo Oktoba 18 mwaka jana kwa kumvamia
Shukrani Habibu na kumnyang’anya simu ya Tecno yenye thamani ya Sh
400,000 na kutokomea nayo kusikojulikana.
Hakimu
Maganga akisoma hukumu alisema kutokana na ushahidi uliowasilishwa na
upande wa mashtaka na utetezi, mahakama inamtia hatiani mtuhumiwa huyo
hivyo kumhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko
24.
“Kutokana
na kosa la unyang’anyi ulilolifanya, kwa mujibu wa sheria natoa adhabu
ya kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 24.
“Utachapwa viboko 12 wakati ukiingia na 12 wakati ukitoka na unayo nafasi ya kukata rufaa,”alisema Hakimu Maganga.
0 comments:
Chapisha Maoni