Wanamgambo
wa Kipalestina huko Gaza wamevurumisha makombora kadhaa kusini mwa
Israel jana. Hata hivyo mashambulizi hayo hayakusababisha majeraha,
lakini yameongeza hali ya wasiwasi katika eneo la mpakani.
Taarifa
ya jeshi la Israel ilisema makombora 25 yamevurumishwa kuelekea maeneo
kadhaa nchini Israel, huku mengi yakizuiwa na mfumo wa kuzuia makombora
wa Iron Dome. Polisi walisema makombora kadhaa yameanguka katika maeneo
ya wazi upande wa Israel, lakini hakuna ripoti zozote za majeruhi
zilizotolewa.
Jeshi
lilisema makombora mengine mawili yalifyatuliwa kutokea Gaza baada ya
mfululizo wa kwanza wa makombora, moja limelipuka karibu na jengo la
shule ya chekechea lakini inaaminiwa hakukuwa na mtoto yeyote ndani ya
jengo hilo wakati wa tukio.
Duru
za usalama za Palestina zilisema vifaru vya Israel vimeyashambulia
maeneo ya kufuatilia matukio ya makundi ya Hamas na Islamic Jihad karibu
na mpakani. Msemaji wa jeshi la Israel alisema hana taarifa kuhusu
hujuma hiyo.
Waziri
Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliapa kuchukua hatua kali. "Israel
huchukulia kwa uzito mkubwa mashambulizi dhidi yake na jamii zake
yanayofanywa na Hamas na Islamic Jihad kutokea Ukanda wa Gaza. Jeshi la
Israel litajibu mashambulizi haya kwa nguvu," alisema Netanyahu wakati
wa mkutano kaskazini mwa Israel.
0 comments:
Chapisha Maoni