Majeshi
ya Israel yameushambulia Ukanda wa Gaza baada ya wanamgambo wa
Kipalestina kufanya mashambulizi mapya ya makombora kuelekea kusini mwa
Israel.
Jeshi
la Israeli limefanya mashambulizi katika Ukanda wa Gaza baada ya
wanamgambo hao wa Kipalestina kurusha takriban makombora 28 ndani ya
Israeli, ambayo yaliufyatua mfumo wa kinga dhidi ya silaha wa Israel wa
Iron Dome.
Kundi
la Hamas linalotawala katika Ukanda wa Gaza, na washirika wake wa kundi
dogo la wapiganaji la Islamic Jihad wamethibitisha kwamba kambi zao za
kijeshi zimeshambuliwa kwa mabomu ingawa hakuna watu walioripotiwa
kujeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya Israel.
Mashambulizi ya kutoka Gaza ndiyo ya kwanza kutokea tangu kuanza wimbi jipya la maandamano tarehe 30 Machi.
Waziri
Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amelaani mashambulizi hayo kuilenga
jamii ya Waisraeli kutokea kwenye Ukanda Gaza na amewalaumu wanamgambo
wa Hamas kwa kuchochea vurugu na hali ya wasiwasi.
Msemaji
wa jeshi la Israel Jonathan Conricus amewaambia waandishi wa habari
kwamba mashambulizi hayo ya roketi na mizinga ni makubwa ukilinganisha
na vita vya mwaka 2014 hali kadhalika lilivyokuwa jibu la Israeli.
Msemaji huyo wa jeshi la Israel ameelezea kwamba wameyashambulia malengo zaidi ya 30 ya kijeshi ya mashirika ya kigaidi.
Wakati
huo huo mashua iliyokuwa na wanaharakati 20 wa Kipalestina waliokuwa
wakijaribu kuvunja marufuku ya miaka 11 katika pwani ya Gaza ilizuiwa na
vikosi vya Israeli kwa mujibu wa mratibu wa maandamano hayo.
Israeli
imesema kutokana na sababu za usalama inazizuia boti zote kutoka Gaza
kuvuka eneo la uvuvi lililowekewa marufuku kwa umbali wa kilomita
kadhaa.
Hapo
awali wavuvi wa Gaza walipigwa risasi na majeshi ya Israel kwa sababu
ya kuivunja amri hiyo. Mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo, Adham Abu
Selmeya, amesema manowari za kijeshi nne za Israel zilitumika kuyazuia
maandamano ya mashua maili tisa kutoka pwani.
Mvutano
katika Ukanda wa Gaza umefikia kiwango cha juu katika wiki za hivi
karibuni. Wapalestina zaidi ya 100 waliuawa na majeshi ya Israeli wakati
wa maandamano makubwa yaliyofanyika mpakani mnamo mwezi Machi.
Eneo
la Ukanda wa gaza linakumbwa na hali mbaya ya kiuchumi, kutokana na
uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na vita vilivyotokea mara tatu
kati ya Wanamgambo wa Hamas huko Gaza na Israeli na pia kuna ukosefu
mkubwa wa bidhaa.
Credit: DW
0 comments:
Chapisha Maoni