Burundi
imeonesha kukasirishwa na kitendo cha Serikali ya Ufaransa kupitia
taasisi yake kutoa punda kama zawadi yake kwa wanakijiji wa Gitega
nchini humo.
Punda
hao walionunuliwa nchini Tanzania waliwasilishwa kwa wanakijiji hao
kama sehemu ya mradi wa kuwasaidia wanawake na watoto kusafirisha mazao
ya kilimo, maji pamoja na kuni.
Hata
hivyo, mshauri wa Rais ameitaja zawadi hiyo kama matusi kwa taifa hilo
la Afrika Mashariki, akisema kuwa imebeba ujumbe mbaya kutoka Ufaransa.
Gabby Bugaga, msemaji wa seneti ya Rais pia aliandika ujumbe kwenye Twitter akieleza kuwa, “Ufaransa wanatuchukua kwa punda”.
“Kuweni wakweli, punda ni ishara ya ubora au ubovu,” aliongeza kwenye tweet yake.
Jumapili
iliyopita, Waziri wa kilimo wa Burundi, Deo Guide Rurema aliwataka
watendaji kuhakikisha wanarudisha haraka punda wote waliowasilishwa kama
zawadi kwa wanakijiji, akiongeza kuwa usambazaji wake haukufuata
taratibu.
Alhamisi iliyopita, mradi huo ulizinduliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Burundi, Laurent Delahousse ambaye aliusifia.
Mwanadiplomasia
wa Ulaya ambaye alizungumza na shirika la habari la AFP kwa masharti ya
kutotajwa jina alisema kuwa uamuzi huo wa Burundi ni kulipiza kisasi
kutokana na kauli ya Ufaransa ya hivi karibuni ya kukosoa uendeshwa na
matokeo ya kura za maoni ambayo yanampa nafasi Rais Pierre Nkurunziza
kuongeza mihula miwili itakayokamilika mwaka 2034.
0 comments:
Chapisha Maoni