Mwanaume
mmoja mwenye silaha amefyatua hovyo risasi na kuwaua askari wawilio wa
kike wa jeshi la polisi na raia mmoja Mashariki mwa jiji la Liege nchini
Ubelgiji.
Katika
tukio hilo lililofanyika jana, mtu huyo pia ameripotiwa kumteka
mfanyakazi wa usafi na kumtumia kama kinga, kabla ya kuuawa na askari wa
jeshi la polisi waliofika katika eneo hilo.
Kwa
mujibu wa Shirika la habari la nchini humo la RTBF, mshambuliaji huyo
aliachiwa hivi karibuni kutoka jela kuwa chini ya kipindi cha matazamio
alipokuwa akitumikia kifungo cha makosa ya dawa za kulevya.
Ingawa
bado haijafahamika chanzo cha uamuzi wa mshambuliaji huyo kufanya tukio
la mauaji, Serikali ya Ubelgiji imesema kuwa inalichukulia tukio hilo
kama tukio la kigaidi na kwamba huenda mtu huyo alifundishwa ugaidi
alipokuwa amefungwa jela.
Meya
wa Liege, Willy Demeyer amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji
alipofanya mkutano na waandishi wa habari. Meya huyo amesema kuwa
watatoa msaada wa kisaikolojia na vitendo kwa familia za marehemu.
Muendesha
mashtaka wa Serikali amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya
asubuhi karibu na mgahawa katikati ya jiji hilo. Amesema kuwa
mshambuliaji aliwanyemelea askari, akamchoma kisu askari mmoja na
kumnyang’anya bunduni kabla ya kuanza kufyatua risasi.
0 comments:
Chapisha Maoni