Serikali
inatarajia kuwanyonga wachumba 40 wa wanamgambo wa Dola ya Kiislamu
(IS) kulipiza kisasi kwa wapiganaji hao wa jihadi kuikalia kwa miaka
mitatu ardhi ya Iraq wakati wa mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu
kuuawa kikatili.
Wanawake
hao ambao ni wa kigeni walikiri mahakamani kwamba na wao ni waathirika
wa IS, walipewa dakika 10 kila mmoja kutetea uhai wao kabla ya majaji
kufikia uamuzi wapewe adhabu kali.
Wanawake
hao walishutumiwa na mahakama ya Iraq na raia wa kawaida kwa kuwapa
msaada waume zao wapiganaji waliosababisha maafa katika eneo walilokuwa
wanakalia kuanzia mwaka 2014 hadi 2017.
Mwanamke
mmoja mwenye uraia wa Ufaransa aitwaye Djamila Boutoutao, 29, alidai
kuwa alidhani alikuwa anaolewa na mwanamuziki wa miondoko ya rap.
“Ni
baada ya kuwasili Uturuki kwa ajili ya ‘mapumziko’ ya wiki moja ndipo
nilipogundua ya kuwa mume wangu ni mpiganaji wa kijihadi,” alisema
Djamila.
“Mimi ni mwathirika. Mume wangu alinipiga na kunifungia kwenye pango na watoto wangu nilipokataa kumfuata (hadi Iraq).’
Djamila
ni mmoja wa raia wa Ufaransa wapatao 1,900 na wasafiri wa kigeni
wanaokadiriwa kuwa 40,000 waliosafiri hadi Syria na Iraq kujiunga na
miliki ya khalifa.
Katika
hukumu yake ya hivi karibuni, ambako aliomba asitenganishwe na binti
yake, Djamila aliwaambia waandishi wa habari wa gazeti la The Guardian:
“Nachanganyikiwa hapa. Nakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha jela
maisha. Hakuna anayeniambia chochote, si balozi wetu wala watu ndani ya
gereza.”
“Jamani
nawasihi msiwaache waondoke na binti yangu. Niko tayari kuwapa fedha
endapo mtawasiliana na wazazi wangu. Tafadhali niokoeni.”
Takriban wanawake 40 ndio wamehukumiwa kifo na watu wengine 300 wenye mafungamano na IS wameshauawa.
0 comments:
Chapisha Maoni