Dogo Janja amesema wamelazimika kuhama nyumba hiyo na kwenda kupanga nyumba nyingine ambayo hulipa US Dollar 800 kwa mwezi kutokana na umbali, pili mkewe, Irene alikuwa akisumbuliwa na kumbumbuka za mara kwa mara kuhusu marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.
“Nahisi kama nilikuwa namuona hivi, kwa hiyo nikashindwa, eeeh!! mara nyingi pia nahisi kama anapita hivi,” amesema Irene Uwoya.
“Of cause inaweza kuwa sababu kila akijitahidi inashindikana kwa sababu alikuwa ni mtu tumemzoea sana,” Dogo Janja ameiambia Clouds FM.Marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ alifariki April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam, alikuwa rafiki wa karibu sana na Irene Uwoya.
0 comments:
Chapisha Maoni