Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limesema nyimbo mbili za Diamond, hazijafunguliwa kama inavyodhaniwa.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema nyimbo za Wakawaka na Hallelujah hazijafunguliwa na jambo hilo halina ukweli wowote na kuwataka wananchi kulipuuza.
Kadhalika,
Mngereza ametoa ufafanuzi kwa nini msanii Diamond amekutana na Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu
wake, Juliana Shonza na sio wasanii wengine.
Mngereza ametoa ufafanuzi huo baada ya kusambaa kwa taarifa iliyoeleza msanii huyo kakutana na mawaziri hao.
Baada
ya taarifa hizo, kulizuka gumzo mitandaoni ambapo watu walihoji kwa
nini wakutane na msanii huyo wakati kuna waliofungiwa nyimbo zao kama
yeye na wengine kufungiwa kufanya muziki kwa miezi sita.
Mngereza
amesema hatua hiyo imetokana na majibizano yaliyokuwa yanaendelea kati
ya Diamond na naibu waziri Shonza na ndio sababu iliyowafanya wawili hao
wakutanishwe meza moja ili kuyamaliza.
Akihojiwa
katika kituo cha Redio Times FM, Diamond alisikika akimrushia maneno
moja kwa moja Shonza kuwa amekuwa akiwafungia wasanii nyimbo zao na
kuwafungia wasifanye kazi kwa lengo la kutafuta umaarufu na kuogopa
kutumbuliwa.
Hata
hivyo, kwa upande wake Shonza alisema hayupo tayari kujibizana na
msanii huyo mitandaoni kwa kuwa aliyemfungia si yeye, bali ni serikali
na kumtaka kufuata taratibu kama anaona ameonewa ikiwemo kufika Basata,
Wizarani au kuandika barua, jambo ambalo Diamond alilitekeleza siku ya
Ijumaa.
Akizungumzia
hilo, Mngereza alitaka wananchi waelewe kwamba malumbano hayo ndicho
chanzo cha Diamond kukutana na mawaziri hao na kuwataka kuondoa dhana
kama mtu aliyepewa upendeleo katika sakata la kufungia nyimbo.
Alipoulizwa
kuhusu kukutana na wasanii wengine wenye malalamiko amesema mpaka sasa
hajapata barua yoyote ya wasanii hao kutaka kuonana nao.
0 comments:
Chapisha Maoni