Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu
ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali
zao.
Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na Oparesheni na Doria za
mara kwa mara ili kudhibiti vitendo vya uhalifu pamoja na kuzuia matukio
mbalimbali yakiwemo ya uporaji na ukabaji na kama mtakumbuka siku za
karibuni kulijitokeza vikundi vya uhalifu vilivyojiita majina ya wakorea
weusi, weupe. Hata hivyo kumekuwa na matukio mawili kama ifuatavyo:-
Watuhumiwa wa uhujumu miundombinu ya TANESCO
Mnamo
24.03.2018 majira ya saa 00.15 usiku askari Polisi waliokuwa katika
doria na oparesheni ya kukamata wahalifu huko maeneo ya Mtaa wa Airport
ya Zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya na
katika Doria hiyo walikamatwa vijana kumi na wawili akiwemo kijana mmoja
ambaye alifahamika kwa jina la ALAIN ACHILE [22] Mkazi wa Airport ya zamani.
Mtuhumiwa
huyu pamoja na wenzake baada ya kukamatwa walifikishwa kituo kikuu cha
Polisi Mbeya Mjini na kufunguliwa mashitaka ya UZEMBE NA UKOROFI ambapo
walishikiliwa na kuhojiwa.
Mnamo 25.03.2018 majira ya saa 10.45 asubuhi mtuhumiwa ALAIN ACHILE
alidhaminiwa na ndugu zake na kwenda nyumbani kwao. Ilipofika majira ya
saa 18.00 jioni zilipatikana taarifa kuwa mtuhumiwa huyo amefariki
dunia.
Mara
baada ya taarifa hizo, wananchi wa eneo hilo la Airport ya zamani hasa
vijana walianza kufanya fujo kwa kutuhumu kuwa Polisi wamehusika na kifo
hicho hivyo kwenda nyumbani kwa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa BOAZ
KAZIMOTO [74] Mkazi wa Iyela kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyewaita
Polisi kwenda kumkamata marehemu ALAIN ACHILE na wenzake hivyo
walipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo walianza kuvunja madirisha ya
nyumba yake, Baadaye walikwenda kwenye barabara za mtaa huo na kupanga
mawe barabarani na kuchoma moto meza za wafanyabiashara wa Soko la
Maendeleo.
Halikadhalika
walikwenda Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Iyela na kubomoa milango
yote, kuharibu samani za ofisi na kuharibu baadhi ya nyaraka mbalimbali
za ofisi ambazo hadi sasa thamani yake haijajulikana. Sanjari na hayo
pia walikwenda nyumbani kwa askari aitwaye H.4325 PC YOHANA wa Kikosi
cha Kutuliza Ghasia na kuvunja madirisha ya nyumba yake huku wakitoa
kauli ya kuwa wataichoma moto nyumba hiyo.
Kutokana
na vurugu hizo askari walifika eneo hilo ili kutuliza vurugu hizo
lakini wakati wanafika wananchi hao walianza kurusha mawe ili kuwadhuru
askari waliokwenda eneo hilo.
Kutokana
na vurugu hizo, Gari yenye namba za usajili PT 1987 aina ya Toyota Land
Cruiser Mali ya Polisi Wilaya ya Mbeya mjini ilivunjwa kioo cha mbele
kwa mawe hivyo kulazimu askari kufyatua mabomu ya machozi kutuliza
ghasia hizo.
Aidha katika vurugu hizo watuhumiwa nane [08] wamekamatwa kuhusika na vurugu hizo ambao ni:-
- ELIUD DAUD [22] Mkazi wa Iyela
- BARIKI MASUDI [30] Mkazi wa Iyela
- FRANK KILEMI [33] Mkazi wa Airport ya zamani
- KRIST NELSON [33] Mkazi wa Airport ya zamani
- ESTOM MBALO [24] Mkazi wa Airport ya zamani
- ROBERT MWANGUPILI [24] Mkazi wa Iyela
- ISSA NELSON [26] Mkazi wa Iyela
- FELIX MBILINYI [21] Mkazi wa Airport ya zamani.
Watuhumiwa
hao wanahojiwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa Mahakamani wakati
wowote mara baada ya taratibu za kisheria zitakapokamilika. Aidha juhudi
ya kuwasaka wengine waliohusika na kuanzisha vurugu hizo zinaendelea.
Nichukue
nafasi hii kuwapa pole wazazi, ndugu na hata walioguswa na kifo cha
kijana huyu, niwathibitishie wananchi kuwa Jeshi la Polisi halikuhusika
na kifo cha kijana huyu kwa aina yoyote. Aidha nimefungua jalada la
uchunguzi [PE] kupitia Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
[RCO] ofisini kwangu kwa ajili ya uchunguzi wa kifo cha ALLAIN ACHILE.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WALIOINGILIA MIUNDOMBINU YA TANESCO.
Mnamo
tarehe 23/03/2018 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na
maafisa wa Tanesco lilifanya Oparesheni katika maeneo ya vijiji vya
Isebe na Isajilo vilivyopo Wilaya ya Rungwe kufuatia taarifa za siri
toka kwa raia wema kuwa kuna watu wanaingilia miundombinu ya Tanesco
katika vijiji hivyo pamoja na kufanya wizi wa nguzo za umeme na
kuwaunganishia umeme wakazi wa maeneo hayo kinyume cha sheria.
Katika
Oparesheni hiyo, watuhumiwa wanne [04] wamekamatwa kwa kosa la
kuingilia miundombinu ya Shirika la Umeme [Tanesco]. Watuhumiwa
waliokamatwa ni:-
- IDD HAMIS MWAMBUSYE [31] Mkazi wa Bagamoyo.
- BENARD KIBONDI [40] Mkazi wa Kikota
- THOBIAS WILFRED [42] Mkazi wa Iponjola
- Eng.GEOFREY MSUNGA [30] Mkazi wa Mbeya
Aidha
miongoni mwa watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa majumbani
kwao walikutwa na vifaa mbalimbali vya umeme ambavyo ni:-
- Mita za umeme 27 aina ya Tropical
- Nyanya za umeme mkubwa na mdogo za aina mbalimbali
- Kitoboleo cha nguzo
- Stay Insulator
- Plaizi
- Tester za umeme
- Seal za mita za umeme
- Vibao vya tahadhari vinavyobandikwa kwenye nguzo za umeme
- Nguzo 57 za umeme ambazo walikuwa zikitumika kuwaunganishia umeme wananchi.
Watuhumiwa
watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika. Aidha
msako mkali unaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaojihusisha na
uhujumu wa miundombinu ya Shirika la Umeme – TANESCO katika maeneo
mbalimbali.
WITO:
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA
anatoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na
badala yake wafuate taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kutii sheria
bila shuruti.
Aidha
anatoa wito kwa jamii kuachana na tamaa ya mali hasa kwa kujihusisha na
vitendo vya kihalifu ili wapate mali na badala yake wafanye kazi
halali.
0 comments:
Chapisha Maoni