Hukumu
ya kesi ya Tito Machibya (maarufu Nabii Tito), ambayo ilikuwa itolewe
uamuzi jana, iliahirishwa hadi Aprili 20, mwaka huu kutokana na hakimu
anayehusika na kesi hiyo kuwa na dharura.
Akitoa
maelezo mahakamani hapo, Mwanasheria wa Serikali Judith Mwakyusa, mbele
ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya, Godfrey Pius, alisema kesi
hiyo ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo.
Mwakyusa
alisema kesi hiyo ilikuwa itolewe uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha, lakini
amepata dharura.
“Mheshimiwa
Hakimu shauri hili limeletwa kwako kwa ajili ya kuahirishwa kutokana na
Karayemaha kuwa na dharura,” alisema.Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo,
Godfrey Pius, aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20, mwaka huu
itakapoletwa tena kwa ajili ya uamuzi.
Pius alisema mtuhumiwa atarudishwa rumande hadi tarehe hiyo.
Aprili
5, mwaka huu Hakimu Karayemaha alisema wamepokea taarifa ya kitabibu
kutoka taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga inayomhusu Mchibya na
uamuzi ungetolewa jana.
Nabii
Tito alidai ana matatizo ya akili yaliyosababisha kutaka kujiua na
kuiomba mahakama kuamuru akachukuliwe vipimo ili kupata uhakika wa afya
yake ya akili.
Katika
kesi hiyo, anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe
na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo, Januari 25, mwaka huu katika mtaa
huo wa Ng’ong’ona alipokwenda kukamatwa na polisi.


0 comments:
Chapisha Maoni