Rais
John Magufuli ametuma salamu za rambirambi za kifo cha mkuu wa mkoa
mstaafu, Abbas Kandoro akisema Taifa limepoteza mtu muhimu ambaye
mchango wake hautasahaulika.
Taarifa
ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa aliyoitoa leo
Aprili 28, 2018 amesema Rais Magufuli Kandoro alikuwa kiongozi shupavu,
aliyejiamini na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na
taratibu, aliwapenda watu aliowaongoza na alidhirisha uzalendo wa kweli.
“Nimepokea
kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Mkoa mstaafu Abbas Kandoro,
nawapa pole wana familia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na
msiba huu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:
“Tumempoteza
mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi kwa umma katika nyadhifa
mbalimbali zikiwemo mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa
halmashauri hautasahaulika.”
Rais
Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza kufikisha
salamu hizo kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote
walioguswa na msiba huo.
“Nimesikitishwa
sana na kifo chake, nawaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira,
uvumilivu na ustahilivu katika kipindi hiki cha majonzi na pia namuombea
marehemu Abbas Kandoro apumzike mahali pema peponi, Amina,” amesema
Rais Magufuli
Enzi za utumishi wake, Kandoro amehudumu mikoa ya Tabora, Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.
Kandoro
alifariki jana Aprili 27, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) na anatarajiwa kuzikwa kesho Aprili 29, 2018 mkoani Iringa.
0 comments:
Chapisha Maoni