Afisa
habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameweka wazi kuwa yeye ni maarufu
zaidi nchini Tanzania kuliko Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey
Polepole.
Haji
Manara amesema kuwa yeye ni kada mzuri wa CCM na Polepole anafanya kazi
kama yake lakini hana jina kubwa kumzidi yeye kutokana na historia ya
maisha yake na chama hicho.
Manara
amedai kuwa CCM ndio chama kilichomsomesha nje ya nchi kuhusu masuala
ya propaganda na ameshawahi kuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es salaam
miaka ya 2007/10.
“Kwa
upande wa siasa mimi ni mwanachama wa CCM haswa, nilikuwa Katibu
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam uongozi wangu ulikuwa 2007/10
" Ilitokea tatizo ambalo ilibidi ifunguliwe kesi ya jinai kwangu, ilivyotokea nikafikiri 2010 tunaelekea kwenye uchaguzi na mimi ni msemaji wa chama changu cha CCM ndani ya Mkoa ndipo nikaamua kuandika barua ya kujiuzulu,“ameeleza Haji Manara kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV na kumtaja Polepole.

“Wote
ni Makada wa CCM ila mimi ni maarufu zaidi, sisemi kwa kudhihaki mimi
na Humphrey Polepole mimi maarufu, mimi ni kada wa chama cha mapinduzi
na nimesomeshwa na CCM kwa wachina, kuhusu Propaganda na nikikuambia
hiki kikombe ni Kamera lazima utakubali ,“amesema Haji Manara.
0 comments:
Chapisha Maoni