Kloof Road House imeingia kwenye orodha ya majumba yenye ubora zaidi duniani na ikielezwa kuwa ni nyumba inayoongoza kwa uzuri na bora zaidi kutoka Afrika. Jumba hili limejengwa nchini Afrika Kusini katika jiji la Johannesbourg.
Nyumba hii imejengwa na kampuni ya Nico van der Meulen architects ambayo imehusika kwenye ubunifu wa majengo mengi sehemu tofauti duniani na inapatikana kwenye mji wa Bedfordview, Johannesbourg imekuwa inawashangaza watu wengi kutokana na jinsi ilivyopangiliwa ndani yake, pamoja na ukubwa wa eneo ilipojengwa likiwa na mita za mraba elfu moja na mia moja.