Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika kesi mbili tofauti.
Kesi ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”
Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano Septemba Mosi kinyume cha sheria.
Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali, Vincent Njau kuzuia dhamana kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.
Baadaye vurugu ziliibuka mahakamani wakati polisi wanataka kumpeleka Lema magereza kwa madai kuwa wanadhani wamechelewa, lakini mbunge huyo alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.