test

Jumapili, 17 Februari 2019

DAWA 6 ZINAZO TIBU TATIZO LA MWILI KUFA GANZI


Dawa-mbadala-6-zinazotibu-ganzi-mikononi-na-miguuni-520x245

DAWA MBADALA 6 ZINAZOTIBU GANZI MIKONONI NA MIGUUNI

Ganzi mikononi na miguuni inamaanisha kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana sababu kunakuwa hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano ya moja kwa moja na ubongo.

Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana miaka ya hivi karibuni.

Kinachosababisha ganzi mwilini ni pamoja na:

1. Shinikizo la muda mrefu kwenye miguu na mikono
2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu
3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva
4. Ajali kwenye neva
5. Kunywa pombe kupita kiasi
6. Uvutaji wa sigara na bangi
7. Uchovu sugu
8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara
9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu
10. Ugonjwa wa kisukari nk

Kwa kawaida ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote lakini onana na daktari mapema ikiwa inakutokea mara kwa mara na pia ikiwa inakutokea na kudumu kwa muda mrefu. Inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa fulani ambao unahitaji matibabu ya haraka.

Kuumwa ganzi kwenye miguu na mikono yako linaweza kuwa ni jambo linaloudhi sana hata hivyo hapa mimi leo nimekuandalia dawa za asili unazoweza kuzitumia kuondokana na tatizo hili.

Endelea kusoma …

Dawa mbadala zinazotibu tatizo la ganzi mwilini:

1. Massaji

Kufanya mazoezi ya massaji wakati unapopatwa na ganzi ni namna nzuri ya kutibu ganzi. Massaji inaongeza msukumo na mzunguko wa damu jambo ambalo mwisho ni tiba kwa tatizo la ganzi. Zaidi masaji inasaidia kusisimua neva na misuli na hivyo kuimarisha na kuongeza mzunguko wa damu kwa ujumla.

*Kwa matokeo ya uhakika weka mafuta ya nazi au ya zeituni au ya mharadali (mustard oil) kwenye viganja vya mikono yako .

*Pakaa sehemu unapopata ganzi

*Massaji maeneo hayo na mikono yako kwa dakika 5 mpaka 7 hivi

*Fanya mara 3 hata 5 kwa siku.

2. Mazoezi ya viungo

Mazoezi husaidia kuimarisha mzunguko wa damu na kuongeza oksijeni sehemu zote za mwili na hivyo kuzuia mwili kupata ganzi.

Mazoezi ndiyo namna pekee ya bure ya kujikinga na kujitibu na magonjwa mengi ikiwemo tatizo la mwili kupatwa na ganzi.

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO GANZI AU ASIDI KUZIDI MWILINI

Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyuwe wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Nyanyuka na ujipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5

Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.

Mazoezi ya kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea ni mazuri pia.

3. Bizari

Bizari au manjano ambayo hujulikana kwa kiingereza kama ‘Turmeric’ ina kitu mhimu ndani yake kijulikanacho kama ‘curcumin’ ambacho husaidia kuongeza msukumo wa damu sehemu yote ya mwili wako.

Pamoja na hiyo pia bizari husaidia kuondoa maumivu na hali ya kutokujisikia vizuri katika mwili wako.

Ongeza kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa bizari ndani ya kikombe cha maziwa ya uvuguvugu ongeza kiasi kidogo cha asali na unywe kutwa mara 1.

Unaweza pia kutengeneza uji mzito (paste) wa bizari na maji na utumie kufanya massaji sehemu unapopata ganzi.

4. Mdalasini

Mdalasini una kemikali na viinilishe mbalimbali ikiwemo manganizi na potasiamu na vitamini nyingi za kundi B.

Faida zake za kiafya zinajumuisha pia kuongeza msukumo wa damu kwenye miguu na mikono yako na hivyo kusadia kutibu tatizo la ganzi. Wataalamu wa tiba asili wanashauri gramu 2 mpaka 4 za unga wa mdalasini zitumike kila siku kwa ajili ya kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai ya mdalasini ya unga katika glasi ya maji ya moto na unywe yote mara moja kwa siku.

Au changanya kijiko kimoja kidogo cha chai cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kingine cha asali na ulambe mchanganyiko huu kila siku asubuhi kwa wiki kadhaa.

Angalizo kuhusu mdalasini feki:

Kabla sijakuacha, ni mhimu sana nikueleweshe juu ya mdalasini hasa ambao hutumika kama dawa. Siyo kila mdalasini unaouona unaweza kukupa maajabu haya, mwingine ni sumu kabisa mwilini. Na watu wengi hawajuwi hili jambo.

(a) Ceylon cinnamon

Mdalasini ambao hutumika kama dawa hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Ceylon cinnamon’ na kwa kawaida wenyewe huuzwa gharama sana. Huwa na radha tamu na harufu ya kuvutia zaidi, unatoka katika nchi ya Sri Lanka katika mmea ujulikanao kama Cinnamon Zeylanicum. Hujulikana pia kama mdalasini wa India.

Huwa na rangi ya kahawia (light brown), mwembamba na mlaini.

(b) Cassia cinnamon

Wakati ule ambao ni feki na ni sumu pia hujulikana kama ‘Cassia cinnamon’ ni mdalasini huu ambao katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku kutumika wala kuingizwa nchini mwao. Hujulikana pia kama mdalasini wa China na wengine huuitwa Saigon.

Mdalasini huu unatoka katika nchi za China, Vietnam na Indonesia. Wenyewe huwa una joto zaidi na huwa na radha kali nay a kuwasha ukiutumia. Madhara yake ni pamoja na kudhuru Ini na figo ukitumika kwa kipindi kirefu.

Cassia cinnamon huuzwa bei rahisi sana na mwingi unaopatikana huko masokoni ni huu. Huwa na rangi inayokaribia na uweusi.

Kwa kawaida ni vigumu kutofautisha aina hizi mbili za mdalasini ukishakuwa tayari katika mfumo wa unga tofauti na ukiwa bado katika fimbo au magome. Mhimu tu ni ununuwe kutoka kwa mtu unayemuamini zaidi.

5. Kula zaidi vyakula vyenye vitamini B

Ili kuzuia ganzi mwilini hasa kwenye mikono na miguu ni mhimu kwamba unakula vyakula zaidi vyenye vitamini B kwa wingi hasa vitamini B6 na B12.

Vitamini hizi ni mhimu kwa ajili ya afya nzuri katika kuzipa neva uwezo wa kufanya kazi vizuri na upungufu wake unaweza kusababisha ganzi katika sehemu mbalimbali za mwili kama kwenye mikono, vidole, na miguu.

Vyakula hivyo ni pamoja na mayai (mayai ya kuku wa kienyeji), parachichi, nyama, maharage, samaki, maziwa, mtindi, mbegu mbegu nk

Unaweza pia kutumia vitamini B-complex mara 2 kwa siku kila siku. Kwa dozi sahihi zaidi muulize daktari wako wa karibu.

6. Ongeza matumizi ya magnesiamu

Usawa mdogo wa magnesiamu katika mwili ni moja ya sababu ya kutokea kwa ganzi katika sehemu mbalimbali za mwili. Magnesiamu ni madini mhimu katika kuwezesha ufanyaji kazi ulio mzuri wa neva za mwili na mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Kula vyakula vyenye magnesiamu zaidi kama vile mboga majani zenye rangi ya kijani, mbegu mbegu, siagi ya karanga, soya, parachichi, ndizi, chokoleti nyeusi, na mtindi wenye mafuta kidogo.

Unaweza pia kutumia viinilishe vya magnesiamu gramu 350 kila siku ila ongea kwanza na daktari wako wa karibu.

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia

1. Kuwa bize na mazoezi kila siku
2. Usikae muda mrefu kwenye kiti
3. Epuka chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine vyote vyenye kaffeina
4. Kula zaidi matunda na mboga za majani
5. Kunywa maji mengi kila siku kidogo kidogo kutwa nzima
6. Epuka sigara na bidhaa nyingine za tumbaku
7. Vaa viatu ambavyo ni saizi yako pia epuka viatu vyenye visigino virefu zaidi
8. Hakikisha una uzito sahihi na siyo uliozidi

Mawasiliano zaidi: WhatsApp +255769142586

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya uwapendao

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni