Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb)
anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Ruvuma
kuanzia tarehe 23 - 25 Novemba, 2017.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 22 Novemba 2017 na Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu atawasili
mjini Songea siku ya Alhamisi tarehe 23 Novemba, 2017 na kupokelewa na
viongozi wa Chama na Serikali katika Uwanja wa ndege Songea majira ya
7.00 mchana.
Baada
ya kuwasili atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na ile ya Chama
Tawala Uwanja wa Ndege Songea. Kisha ataelekea Wilaya ya Namtumbo ambapo
atafungua ghala la MIVARF, kuongea na Madiwani na watumishi wa Umma na
baadaye ataongea na wananchi wa Namtumbo kwenye mkutano wa hadhara.
Ijumaa
tarehe 24 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu ataendelea na ziara yake
kwa kuongea na wananchi wa kijiji cha Mchomoro kisha ataelekea Wilaya
ya Tunduru ambapo atasalimia na wananchi wa vijiji vya Rahaleo,Milonde
na Matemanga akiwa njiani kuelekea mjini Tunduru.
Aidha,
Mheshimiwa Waziri Mkuu atatembelea kituo cha Afya cha Nakayaya, ghala
la kuhifadhia Korosho na kupata taarifa ya Chama Kikuu Cha Ushirika
TAMCU. Jioni Mheshimiwa Waziri Mkuu ataongea na wananchi kwenye mkutano
wa hadhara utakaofanyika mjini Tunduru katika uwanja wa michezo.
Jumamosi tarehe 25 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu atahitimisha
ziara yake mkoani Ruvuma na kurejea Dar es Salaam
Mkuu
wa Mkoa Mndeme ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma
kujitokeza kwa wingi katika mapokezi kuanzia uwanja wa Ndege Songea
atakapowasili Aidha amewaomba wananchi kujitokeza kwenye maeneo yote
ambayo Waziri Mkuu atapita na kwenye mikutano ya hadhara ili wapate
fursa nzuri ya kumsikiliza Mheshimiwa Waziri Mkuu na kupokea maelekezo
atakayoyatoa.
0 comments:
Chapisha Maoni