test

Jumatatu, 29 Agosti 2016

Hii ndio moja ya ndege mpya ya Air Tanzania iliyo tayari kwa kila kitu.....PONGEZI KWA SERIKALI HII YA AWAMU YA TANO


Hii ndio moja ya ndege mpya ya Air Tanzania iliyo tayari kwa kila kitu.Hapa ipo kwenye Hangar(eneo la matengenezo ya ndege) nchini Canada tayari kwa kuanza safari ya kuja Tanzania.Wakati wowote na siku itakayotajwa ya mwanzoni mwa mwezi September ndege hizi mbili zitatuwa katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dsm.

Katika picha ni ndege hiyo ikiwa na rangi ya ATCL na picha nyingine ni kabla ya kuwa na rangi yoyote ya kampuni na nembo.Nchini Canada ndege hiyo imepewa Reg # ya C-FIFG...kwa mujibu wa ICAO kila nchi huwa na usajili wake tofauti,mfano kwa ndege zote zilizosajiliwa Kenya lazima zianze na 5Y-(then hufuata herufi za ndege husika ambazo hazitafanana na ndege nyingine yoyote)-,ndege zilizosajiliwa Uganda huanza na 5X-..ndege zenye usajili wa Afrika Kusini huanza na ZS- na hivyo ndege zenye usajili wa Canada huanza na 5H-,nilitembelea Kigali,wao huanza na 9XR-..


Hivyo ndege hii ambayo Tanzania imenunua huko Canada ilitambulika kwa usajili wa C-FIFG,na hivyo itakavyotua Tanzania itabidi tubadili na tuipe usajili wa Tanzania utakaoanza na 5H- .

Kwa hili nimpe hongera Rais Magufuli na Serikali yake,kwani hakika ukiangalia historia ya ndege hii ina mwaka mmoja tu toka ianze kutengenezwa kiwandani.Lakini pia ukiangalia flight movement records zake inaonyesha imeruka Mwezi August 2016 kwa muda wa saa moja na dakika tisa kama sehemu ya majaribio.Hii ni dalili kuwa tunaenda kuwa na ndege mpyaaa,ingekuwa enzi za ujana wetu miaka ya 80 tungesema "ndege mmaaaaaa"!!PONGEZI KWA SERIKALI HII YA AWAMU YA TANO.

Nimeambatanisha "details" za ndege hiyo,ambapo ili watu wasione tumeingizwa chaka bado ina Reg# ya Canada ambayo sisi tutaibadilisha vile tunavyotaka.Hakika ndege hizi ni rafiki kwa mazingira ya viwanja vya Tanzania na usafiri wa ndani.Itasaidia kutua hata katika viwanja "korofi" kama Mtwara,Kigoma,Tabora,Iringa,Songea,Dodoma(japo nasikia inafanyiwa ukarabati) na viwanja vingine kama Arusha,Mwanza,Znz,Tanga na Mbeya.
WELCOME TO THE MARKET ATCL.....THE WINGS OF THE KILIMANJARO image.jpeg image.jpeg

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx