Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri ametupilia mbali
pingamizi la viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe la kutaka kesi ya
kufanya maandamano ifutwe badala yake ameagiza hati ya mashtaka ya kesi
hiyo ifanyiwe marekebisho.
Mashauri
amesema amekubaliana na hoja 2 za upande wa mashtaka kati ya hoja 8
ambazo ziliwakilishwa Mahakamani na upande wa mashtaka.
Hata
hivyo, upande wa utetezi kupitia wakili wao, Peter Kibatala umetangaza
nia ya kutoridhika na maamuzi hayo yaliyotolewa na Hakimu na kudai
kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
Wakili
wa serikali Mkuu, Paul Kadushi umedai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya
Mahakama za Mahakimu hakuna uwezekano wa kukata rufaa katika uamuzi
mdogo ambao hauwezi kuathiri kesi.
“Naomba mahakama ipuuzie hoja hizo na nia hiyo ni batili,”ameeleza Kadushi.
Uamuzi
juu ya rufaa ya kesi hiyo umetangazwa kutolewa June 12, 2018 na Hakimu
Mkazi Mashauri baada ya mvutano mkali kati ya pande hizo mbili.
Washtakiwa
wa kesi hiyo ni viongozi wa nyadhifa kubwa katika chama cha upinzani
Chadema akiwemo, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Mbunge
wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu
na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, Mbunge wa
Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji,
Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa Tarime vijijini, John Heche na
mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112
ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali
kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama
maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina.
0 comments:
Chapisha Maoni