Baada
ya Tanzania kuibuka kinara wa Uchumi Jumuishi barani Afrika, baadhi ya
Wataalamu wa masuala ya uchumi nchini wameelezea kuwa hatua
zinazochikuliwa na Serikali kuwawezesha wanachi kuwekeza katika shughuli
za kiuchumi na utoaji bora wa huduma za jamii vitaufanya uchumi wa
Tanzania kuendelea kukua zaidi.
Wakitoa
maoni yao juu ya dhana ya uchumi jumuishi, baadhi ya wataalamu hao
wamesema kuwa madiliko ya sera na sheria zinawawezesha wananchi wengi
kumiliki uchumi ni sehemu ya vigezo vya kuufanya uchumi kukua huku
ukigusa maisha ya wananchi walio wengi.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi, Bi. Bengi Issa
ameielezea dhana ya uchumi jumuishi kuwa ni ile ambayo shughuli za
kiuchumi zinawajumuisha moja kwa moja wananchi na kwamba mabadiliko ya
sheria katika sekta ya madini na katika umiliki wa makampuni ya simu
yametoa fursa kwa watanzania wengi kushirikikatika uchumi.
Amesema
kuwa utekelezaji wa sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi
kidato cha nne, kuimarishwa kwa huduma za afya, maji, umeme pamoja na
mapambano dhidi ya rushwa, hifadhi ya jamii na utekelezaji wa miradi
ambayo inawapa fursa wananchi kushirikikatika shughli a kiuchumi ni
miongoni mwa sifa zinazoifanya Tanzania kushika nafasi ya juu.
“Serikali
inaweka mazingira bora ya wananchi kushiriki shughuli za kiuchumi
katika miradi mbalimbali. Tunahakikisha kila mradi unaoingia nchini basi
wafanyabiashara wa Tanzania wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji
wa mradi huo”, alifafanua Bi. Bengi.
Amesema
kwa upande wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi wamekuwa
wakishiriki katika kuweka mipango na sera ili kuhakikisha Watanzania
wengi wanashiriki shughuli zakiuchumi ikiwemo kumiliki ardhi ili
iwasaidie katika kutafuta mitaji ya biashara.
Nae
Mtaalam wa Uchumi wa Kilimo ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa
Taasisi ya ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo anaeleza kuwa mfumo bora wa
utawala nchini umewezesha Tanzania kuwa na Uchumi Jumuishi kutokana na
wananchi kuanzia ngazi ya kijiji kushirikishwa katika kupanga mipango ya
maendeleo jambo ambalo linawafanya waangalie vipaumbele muhimu katika
maeneo yao.
Dkt.
Lunogelo anataja mradi ya TASAF, kuongezeka kwa mikopo kwa wanafunzi
wa elimu ya juu, kuanzishwa kwa vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS)
na kurahisishwa kwa huduma za kifedha ni miongoni mwa mambo yanaifanya
Tanzania kuibuka kinara katika uchumi jumuishi.
Aidha,
Dkt. Lunogelo anaeleza kuwa kutokana na kuendelea kuboreshwa kwa mifumo
na juhudi za makusudi za Serikali za kuwasaidia Watanzania wengi zaidi
kushiriki shughuli za kiuchumi kutaifanya Tanzania kung’ara zaidi katika
suala la uchumi jumuishi ambao unafaidisha wananchi wengi.
“Uchumi
jumuishi ndio msingi mkubwa wa kuleta amani na utulivu katika nchi
kwani watu wanaguswa na matunda ya ukuaji wa uchumi”, alieleza Mtaalamu
huyo wa Uchumi.
Dkt.
Lunogelo anasisitiza kuendelea kufanya kuwashirikisha na kuwatafutia
wananchi fursa zaidi za kiuchumi ili dhana hii ya Uchumi Jumuishi
iwaguse Watanzania wengi zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni