Na Mathias Canal, WK-Tabora
Waziri
wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amepiga marufuku kwa wanunuzi wa pamba
kuondosha pamba ya wakulima kwa maelewano ya kulipa baada ya siku
kadhaa badala yake ameagiza wakulima wa pamba kulipwa fedha zao kabla ya
pamba kusafirishwa.
Dkt
Tizeba amepiga marufuku hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja
mkoani Tabora jana 11 Juni 2018 wakati akihutubia wakulima wa pamba
katika kijiji cha Mulidede na Ishihimulua vilivyopo katika Wilaya ya
Uyui sambamba na kijiji cha Miguwa kilichopo katika Wilaya ya Nzega.
Dkt
Tizeba alisema kuwa kumekuwa na ombwe la wakulima kucheleweshewa malipo
yao baada ya kupeleka pamba kwenye kampuni za ununuzi jambo ambalo
linachelewesha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wakulima hao na
familia zao kwa ujumla kwa wakati tarajiwa.
Alisisitiza
kuwa ili pamba iweze kusafirishwa kwenda popote baada ya mauziano ni
lazima mkulimwa alipwe stahiki zake kwa wakati sio kuishi kwa kukopesha
bidhaa hiyo muhimu isiyokuwa na uduni wa soko.
Dkt
Tizeba amemaliza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora akitokea mkoa wa
Singida ambapo pamoja na mambo mengine anakutana na wakulima na
wanunuzi wa pamba ili kujionea zoezi la ununuzi na uuzaji wa pamba.
“Lakini
ndugu zangu wakulima na ninyi ni lazima niwaambie ukweli baada ya kuuza
pamba mnapaswa kuwa makini katika matumizi ya fedha zenu kwani endapo
mkitumia hovyo vile vile fedha hizo zitamalizika pasina kufanya jambo la
maendeleo kwa familia na jamii kwa ujumla” Alikaririwa Dkt Tizeba
Katika
hatua nyingine Dkt Tizeba ametangaza neema kwa wakulima wa pamba kwa
kuwafahamisha kuwa kila mwananchi aliyelima pamba ni mwanachama wa chama
cha ushirika AMKOS hivyo ana sifa za kuchagua au kuchaguliwa kuwa
kiongozi wa chama cha ushirika.
Tayari
waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba amewasili Wilayani Kahama
ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa masoko ya Tumbaku
Kitaifa hafla itakayofanyika katika mkoa wa kitumbaku-Kahama 12 Juni
2018.
MWISHO.
0 comments:
Chapisha Maoni