Waziri
wa Elimu Nchini Afrika Kusini, Angie Motshekga amesikitishwa na kwaya
ya kundi moja la wanafunzi ambao wamekuwa wakiimba wakiwa watupu.
Amesema
kuwa amesikitishwa sana baada ya kuona kanda ya video ya wasichana hao
wa Xhosa wakicheza densi yao huku wakiwa wamevalia nguo inayojulikana
kama “inkciyo”.
Aidha,
Waziri huyo amesema kuwa ni ukosefu wa heshima kwenda kinyume na
maadili ya tamaduni za taifa hilo hasa kwa watoto wa kike.
“Tabia
hiyo mbaya sana inaenda kinyume na maadili ya tamaduni zetu, mtoto wa
kike anafaa kuthaminiwa na si kufundishwa mila potofu,”amesema Waziri
Motshekga
Hata
hivyo, mkufunzi wa Kwaya hiyo ya wanafunzi amesema kuwa ni fahari kubwa
kucheza densi ya kitamaduni ya Xhosa huku wasichana wakiwa watupu.
0 comments:
Chapisha Maoni