Wananchi
wa kijiji na Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wamehoji juu ya shamba
lenye ekari 326 lililofutiwa hatimiliki na Rais, kurudi kwa mmiliki wa
awali.
Walisema
wanashangazwa kuona shamba hilo lililokuwa likimilikiwa na Esther
Sumaye – mke wa Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, likiendelezwa kwa
kilimo, kuchimbwa visiki na kukodishwa kwa wananchi, huku viongozi
wakiwa kimya bila kutoa taarifa yoyote ya mabadiliko ya umiliki wake.
Akizungumza
jana, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kijoja, Ally Saleh, alisema
wameshtushwa na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,
Mohamed Utali kuwa shamba hilo limerudi kwa mmiliki wake wa mwanzo,
Esther kutokana na uamuzi uliotolewa na mahakama baada ya kukata rufaa
na kushinda kwa mujibu wa sheria.
“Tunashangaa
kusikia kwamba eti shamba ambalo liko katikati ya kijiji na
lilirudishwa kwa wananchi na Rais, barua tulipewa, lakini kwa sasa
tunaambiwa kijuujuu tu kuwa limerudi kwa Esther Sumaye bila uthibitisho
wowote,” alisema Saleh.
Nao
wananchi wa kijiji hicho, Said Ally, Said Kibeku na Maila Suteli,
walisema wanalitegemea eneo la shamba hilo kwa maendeleo ya kijiji,
ikiwamo ujenzi wa makazi, viwanda, shule na zahanati kutokana na
kuchukua eneo kubwa.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Utali, alisema halmashauri
ilikuwa katika harakati za kutaka kuligawa shamba hilo kwa wananchi kama
maelekezo ya Serikali yalivyotaka, lakini ilishindikana baada ya
kupokea barua ya kuwa shamba limerudi kwa Esther.
“Tulipokea
barua iliyoambatana na hukumu kutoka kwa mwanasheria wa Esther Sumaye
kuwa mahakama imempa ushindi Esther Sumaye katika kesi namba 25 ya mwaka
2016, hivyo hatuwezi kukurupuka na kuingilia eneo ambalo lina hukumu ya
mahakama,” alisema Utali.
0 comments:
Chapisha Maoni