Mbunge
wa Nzega, Hussein Bashe amefiwa na Mama yake Mzazi, Zainab Abdi
aliyekuwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
jijini Dar es salaam.
Bashe amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kutoa taarifa hiyo.
"Ndugu zangu nimeondokewa na mama yangu mpendwa.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un"
Naye,
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amempa pole Mbunge huyo kwa
kuandika “Inna lilah waina ilaih raajiun. Mola akupe subra ndugu yangu
@HusseinBashe katika mtihani huu mkubwa wa kufiwa na mama yako mzazi.”
Zitto
ameongeza kwa kuandika “Inna lilah waina ilaih raajiun. Mola akupe
subra ndugu yangu Hussein Bashe katika mtihani huu mkubwa wa kufiwa na
mama yako mzazi. Poleni sana Sheikh Mohammed, Ibrahim Mohamed Bashe,
Abubakar, Kauthar na ndugu na jamaa huko Nzega. Tupo pamoja nanyi na
Mola awape nguvu.”
0 comments:
Chapisha Maoni