Mbunge
wa Geita Mjini (CCM), Constantine Kanyasu ameitaka Serikali kulieleza
Bunge ni lini itajenga reli kipande cha Makotopora– Kigoma hadi Mpanda
na baadaye kipande cha Isaka hadi Kigali.
Kanyasu
ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 1, 2018 wakati akiuliza swali la
nyongeza huku akitaja pia ujenzi wa reli ya kisasa katika mikoa ya Geita
na Kagera.
Akijibu
swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta
Nditiye amesema kwa sasa Serikali imeshakamilisha taratibu za ujenzi wa
reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam- Morogoro hadi Makotopora (Dodoma).
“Kuhusu
ujenzi wa kipande cha Geita – Kagera hadi Uganda, mchakato bado
unaendelea na mara fedha zitakapopatikana mbunge atajulishwa,” amesema
Nditiye.
Amesema
Serikali inatambua kila nchi ina wajibu wa kutekeleza mradi wa kujenga
reli hiyo katika sehemu yake, kwamba ni wajibu wa kila nchi kukamilisha
mradi huo ili kuchochea maendeleo yanayotokana na ujenzi wa reli hiyo.
Kuhusu
kipande cha reli ya Isaka kupitia Kabanga hadi Rusumo na Kigali nchini
Rwanda, amesema Serikali inakamilisha maandalizi ya ujenzi wake na
mkataba na usanifu na matayarisho ya zabuni umesainiwa na kazi itaanza
Juni 2018.
0 comments:
Chapisha Maoni