Mkuchika
ametoa kauli hiyo, leo Juni 8, 2018 wakati akijibu swali la Mbunge wa
Viti Maalum(CHADEMA), Ruth Mollel aliyeihoji serikali kuwa, Wakurugenzi
wa Halmashauri ambao wameteuliwa wengi wao walikuwa ni wana CCM
walioshindwa katika kura za maoni na wao ndio wasimamizi wa uchaguzi
kuna wengine kama huyu wa Ubungo anahudhuria vikao vya CCM, Swali langu
ikiwa tutaleta orodha ya Wakurugenzi ambao tunajua ni wana CCM na
walikuwa katika kura za maoni Je serikali itakuwa tayari kuwaondoa?
“Swali
la pili tunao wakuu wa mikoa ambao wanalipwa kwa pesa za walipa kodi
Watanzania wenye vyama na wasiokuwa na vyama lakini wengi wameonyesha
itikadi za kisiasa ukiangalia mkuu wa mkoa Arusha, Mkuu wa Mkoa wa
Manyara na wengine Je, serikali ina kauli gani kuhusu hilo?
Akijibu
swali hilo, Mkuchika amesema kuwa “Mkurugenzi yoyote utakaye mchagua
katika nchi hii lazima kuna Chama anachokipenda, huyu yuko pale baada ya
kuteuliwa kuwa mkurugenzi na Waraka wa utumishi wa umma unasema
Mtumishi wa umma anaeteuliwa na Rais endapo hata ridhia kufanya ile kazi
ana ruksa ya kumuambia Mh. Rais naomba niendelee na kazi yangu , sasa
hao wakurugenzi walipokuwa wanafanya kazi walishakoma kazi waliokuwa
wanaifanya, kazi wanayoifanya ni Ukurugenzi wa Halmashauri nataka niseme
Rais anapoingia madarakani anapanga safu yake.”
Ameongeza,
“Yule wa Ubungo kuhudhuria vikao naomba nisema mkishakuwa mnachama
tawala siku zote kazi yenu nikuihoji serikali , Mkurugenzi wa Ubungo sio
Mjumbe wa CCM lakini anweza kutwa akaelezea utendaji wa ilani ya
uchaguzi katika jimbo la Ubungo.”
Amesisitiza
kuwa “Swali la pili kuhusu wakuu wa mikoa , nataka niseme Wakuu wa
Mikoa wanamuwakilisha Rais, Mkuu wa Mkoa ndio Rais wa Mkoa ule , Rais ni
neno la kiarabu maana yake kichwa kwahiyo kichwa cha mkoa ule ni Mkuu
wa mkoa ule, huyu Mkuu wa Mkoa anamuwakilisha Rais , hutegemei huyu Mkuu
wa mkoa afanya mambo tofauti anayofanya Rais, lakini mwisho nimalizie
kusema kwamba nchi hii tunachombo kinaitwa mahakama muhimili wa mahakama
kazi yake ni kutafsiri sheria , pale mtu anavyoona hakutendewa ndivyo
sivyo basi tufuate mkondo wa sheria na baadhi yao mnaowasema walikuja
hapa kwenye maadili wakasiliza wakawa cleared wakaonekana hawana
makosa.”
0 comments:
Chapisha Maoni