Victoria
Salvatory (58), mkazi wa kata ya Katoma, Kagera anashikiliwa na polisi
kwa tuhuma za kumuua mumewe, Salvatory Iteganira (62) kwa kile
kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi amesema mauaji hayo yalitokea jana saa 6:00 mchana.
Akizungumza
leo Mei 28, Kamanda Ollomi amesema mtuhumiwa anadaiwa kumpiga mumewe
kwa kitu kizito kichwani na kumsababishia jeraha lililovuja damu nyingi
na hatimaye kifo.
“Wanandoa
hao wanadaiwa kuwa na ugomvi ambao chanzo chake tunaendelea kuchunguza;
baada ya ugomvi huo mtuhumiwa alimpiga mume wake kichwani kwa kitu
kizito kilichosababisha jeraha lililovuja damu nyingi na kusababisha
kifo chake,” amesema Ollomi.
Kamanda
huyo amewaasa wanandoa na wapenzi kutumia njia ya majadiliano,
usuluhishi na sheria kutatua tofauti miongoni mwao badala ya
kujichukulia sheria mikononi.
0 comments:
Chapisha Maoni