Katibu
mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameng'atuka
nafasi yake aliyokuwa akiishika ndani ya chama hicho na CCM wameridhia
ombi hilo rasmi.
Hayo
yamewekwa wazi na taarifa zilizotolewa na Katibu wa NEC-Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo Mei 29, 2018 na kusema kwa pamoja
wamemtakia mafanikio mema katika shughuli zake.
"Napenda
kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi
(CCM) na CCM itaendeleaq kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali
ya chama kwa kadiri itakavyohitajika", imesema taarifa hiyo.
Kwa
upande mwingine, Kinana wakati anatoa neno lake la kuwaaga wajumbe wa
NEC amewasisitizia wajumbe hao na wana CCM kiujumla kudumisha umoja wa
wanachama na chama cha mapinduzi (CCM).
0 comments:
Chapisha Maoni